Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Godfrey Mzava, amekagua ujenzi wa mradi wa kiwanda cha makaa ya mawe, kata ya Visegese wilayani Kisarawe, Mkoani Pwani ambao unatekelezwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), ambapo hadi kukamilika kwake utagharimu sh. bilioni 2.4.
Imeelezwa kuwa kati ya fedha hiyo bilioni 1.2 ni kwa ajili ya kununua mtambo na bilioni 1.2 ujenzi na vifaa, unatakiwa kukamilika kabla ya Mei 30, 2024 ambapo umefikia kwenye asilimia 60 bado asilimia 40 na utazalisha tani 20 kwa saa za mkaa mbadala.
Maelekezo hayo yametolewa leo Mei 3,2024 baada ya kukagua kiwanda hicho , Mzava aliwaomba STAMICO kuongeza kasi ya ujenzi ili ukamilike ndani ya siku 27 zilizobakia.
"Agenda yetu ya msingi kabisa katika Mwenge wa Uhuru 2024 kuhusu Uhifadhi wa mazingira na uchaguzi wa Serikali za Mitaa katika Uhifadhi wa mazingira, tunavyokwenda na mabadiliko ya kutoka kwenye nishati isiyo rafiki" alifafanua Mzava.
Nae kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt Seleman Jafo alieleza mradi huo ni muhimu katika kutunza mazingira.
"Tunapoteza hekta zaidi ya laki nne, hii ni changamoto ndio maana Rais Dkt Samia katika mkutano wake alipokuwa na akinamama alihimiza matumizi ya nishati safi ya kupikia,halikadhalika Makamu wa Rais Philip Mpango wakati wa maadhimisho ya STAMICO aliwaelekeza waanze mpango wa kutengeneza nishati mbadala"
Akipokea Mwenge wa Uhuru Mei 3 mwaka huu, eneo la Kiluvya Madukani, ukitokea Kibaha,Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Fatma Nyangasa, alieleza miradi iliyopitiwa ni 7 yenye thamani ya sh. bilioni 3.4.
Kati ya miradi hiyo ni Mradi wa Ujenzi wa Box karavat kata ya Makurunge, mradi wa kupanda miti na kukagua zoezi la upandaji miti shule ya Sekondari Kisarawe na kuzindua jengo la mama na mtoto kata ya Masaki.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.