Mkoa wa Pwani Kupitia wakala wa Nishati Vijijini (REA) umepokea Miradi ya Nishati ya Zaidi ya shilingi Bil. 1.777 ambazo kati yake Zaidi ya Sh. Bil. 1.3 ni za Umeme Jua wenye Teknolojia isiyotumia Nyaya utakaonufaisha Kaya 2,243 na Sh. Milioni 477 za utekelezaji, usambazaji na ugawaji Majiko Banifu 10,650 kwa wananchi.
Akizungumzia mradi wa Majiko Banifu, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amesema ni Jitihada za serkali katika kuhamasisha wananchi kuhusu matumizi ya nishati safi na utunzaji wa mazingia hususan katika kukabiliana na ukataji wa miti ovyo.
Ameeleza kuwa katika miradi hiyo, serikali imetoa ruzuku ya asilima 80 kwa kila mradi ili kuwezesha wananchi kupata huduma hizo kwa gharama nafuu.
Kwa Upande wake Meneja wa Teknolojia za Nishati wa wakala wa Nishati Vijiji - REA Mhandisi Michael Kyssi amesema kwa mkoa wa Pwani majiko 10,650 yatauzwa kwa bei ya Ruzuku ya shilinhi 10,200 kwa jiko moja.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.