Hayo yamesemwa na Mhe Abubakar Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani leo Juni 21 2022 wakati alipokutana na Ugeni kutoka REA Makao Mkuu, TANESCO Makao Makuu na Wawakilisha wa Wafadhili hao European
Union na Wizara ya Nishati.
“REA angalieni Namna ya kushiriki kwenye Mpango Mikakati ya kupanga Mkoa huo Kiuwekezaji" Mkoa wa Pwani ni Mkoa Viwanda una Viwanda 1453 na Viwanda Vikubwa ni 87, vilevile Tuna Maeneo Makubwa ya Uwekezaji Amewaeleza Kunenge.
Kunenge amewaeleza kuwa Umeme unahitajika mwingi lakini hautoshelezi unakatika mara kwa mara. Ameeleza pia Serikali imejenga Vituo vya Afya, Shule na Hospital Vinahitaji Umeme.
Ameeleza kuwa Umeme usiwe kwa kupikia na mwanga pekee tunahitaji kwa Matumizi ya Viwanda Vidogo Vidogo.
Kunenge ameeleza kuwa hadi sasa vimebaki Vijiji 89 kati ya 417 ambayo havijaunganishwa na umeme kwenye Mkoa huo.
"Kwa Sasa wakandarasi wapo maeneo ya Vijiji hivyo kupeleka Umeme" Ameeleza Kunenge.
Naye Eng. Emanuel Yesaya Kutoka REA makao Mkuu na Mathias Roche mwakilishi Muungano wa Nchi za Ulaya European Union ambao ni Wafadhili wa mradi huu wameeleza wamefika Mkoani hapo kuangalia Namna gani Umeme Umewasaidia Wananchi Kujiingiza kwenye Shughuli zingine za Kiuchumi kwa Maeneo ya Bagamoyo Kimarangombe Funta Kihangaiko.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.