Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi. Evarist Ndikilo leo tarehe 20 Aprili 2020 amewahimiza Wananachi wa Mkoa huo kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na Maambukizi ya Virusi vya Corona.
amewahimiza Wananchi wote wa Mkoa huo Kuvaa Barakoa wanapokwenda katika Ofisi mbali mbali za Umma na Binafsi ikiwemo Ofisi yake, kwenye Daladala, Bodaboda na maeneo ya Biashara ikiwemo Sokoni.
Aidha, amewahimiza kunawa kila mara kwa Maji tiririka na Sabuni au kutumia vitakasa Mikono,kukaa umbali wa mita moja na mwezio, na kutoa taarifa pale wanapohisi kuwa wanadalili za Maambukizi ya Virusi vya Corona.
Katika hatua nyingingine Mhandisi Ndikilo amesema kwa kuwa, tayari Mkoa una Mgonjwa mmoja na Mkoa Pwani upo karibu na Dar es salaam penye wagonjwa wengi amewataka Wananchi kujilinda kwa kuchukua tahadhari zote Muhimu.
Mhandisi Ndikilo ameyasema hayo katika ziara fupi Wilayani Kibaha (Sokoni, Stendi na Maeneo ya Biashara) iliyolenga kukagua utekelezaji wa tahadhari zinazotolewa katika Kuthibiti maambukizi ya Virusi vya Corona.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.