Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mhandisi Evarist Ndikilo amepokea Mwenge wa Uhuru ,ukitokea jijini Dar es salaam ,ambapo ukiwa mkoani hapo Mwenge wa unatarajiwa kupitia miradi ya maendeleo 67 yenye thamani ya sh.bilioni 162.4(Bilion mia moja sitini na mbili na mia nne arobain million na elfu nane mia saba sabini na tatu. .
Kati ya miradi hiyo , miradi16 itawekwa mawe ya msingi ,miradi 13 itazinduliwa ,na Miradi 8tafunguliwa na 21 itakaguliwa.
Mhandisi Ndikilo alisema kuwa ,Mwenge wa uhuru ukiwa Mkoani hapa, pia utapitia katika Wilaya zake 7 na Halmashauri zote 9.
Alisema Mwenge wa Uhuru utapokea taarifa ya miradi 9 katika maeneo mbalimbali ya mkoa hapa na wamehakikisha kuwa miradi yote itakuwa na thamani ya fedha iliyotajwa.
Aidha alieleza kuwa ,miradi hiyo imetekelezwa kwa ushirikiano baina ya Wananchi,Serikali kuu,Halmashauri na wahisani wa Kitaifa na kimataifa.
” Kaulimbiu ya mbio za Mwenge kwa mwaka huu ni ‘Elimu ni ufunguo wa maisha, wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu.’
“Katika kutekeleza ujumbe huo tumejipanga kutekeleza kwa vitendo ambapo kwenye elimu tumevuka lengo kwa kuandikisha watoto wa darasa la kwanza.” alisema Ndikilo.
Mkuu huyo wa mkoa alieleza ,mwaka huu lengo ilikuwa 47,686 walioandikishwa ni 52,551 sawa na asilimia 110. Alisema Mhandisi Ndikilo
Katika hatua nyingine Ndikilo alisema ,katika upande wa viwanda wamefanya kazi nzuri kwani kwasasa Mkoa wa Pwani una viwanda zaidi ya 400 kati ya hivyo vipo vikubwa ,vya kati na vidogo.
“Asilimia 20 ya ajira zote viwandani Pwani ni za wazawa wa mkoa na wanatarajia kufikia asilimia 50.” alielezea Ndikilo.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu Charles Kabeho, alihimiza elimu kwa watoto wote huku akiwahimiza wazazi kuwa na mwamko wa kuwapeleka watoto shule.
Mwenge huo umeanza mbio zake July 12 wilayani Mkuranga Mkoani Pwani na July 13 unatarajiwa kupokelewa wilayani Rufiji
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.