Mwenge wa Uhuru umezindua huduma ya upasuaji katika Hospitali ya Wilaya ya Kibaha ambayo inakwenda kuondoa adha ya wananchi ya kusafiri umbali wa km 40 kufuata huduma hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi.
Akitoa taarifa hiyo Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo Dk. Christopher Ngendello ameeleza kwamba Hospitali hiyo ilipokea sh Miln 300 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya Ununuzi wa vifaa tiba vya uchunguzi vya upasuaji.
Alisema vifaa vilivyonunuliwa ni pamoja na Mashine ya usingizi, vitanda 30, Mashine ya kemia, magodoro 30, , makabati ya dawa, jokofi za kuhifadhia damu viti vya kuchangia damu na vifaa vya upasuaji.
Dk.Ngendelo alisema huduma hiyo imeanza kutolewa mwezi Machi mwaka huu na hadi kufikia April 8 wagonjwa 16 wamefikia kupata huduma hiyo
""Kutolewa kwa huduma ya upasuaji katika Hospitali ya Wilaya kumesaidia kusogezwa kwa huduma karibu na wananchi pia inepunguza gharama ya sh.miln 24 hadi 30 zilizokuwa zinatumika kununua mafuta na matengenezo ya magari ya kubebea wagonjwa," alisema.
Akizindua mradi huo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Ismail Ussi aliipongeza Serikali kwa namna inavyowajali wananchi wa hali ya chini na wahali ya juu katika kuwasogezea huduma za afya karibu na wanakoishi.
Ussi aliwataka Wananchi kutunza majengo ya Hospitali hiyo hiyo huku akiwasisitiza kuyatumia kupata huduma ambazo zinatolewa badala ya kuendelea kusafiri mbali.
Kadhalika Kiongozi huyo aliwataka wananchi kupambana na magonjwa ya Malaria na Ukimwi kwa kuzingatia elimu inayotolewa na wataalamu wa afya kutokomeza magonjwa hayo.
Akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka Wilaya ya Bagamoyo , Mkuu wa wilaya ya Kibaha Nickson Saimoni alisema mwenge wa uhuru ukiwa katika wilaya hiyo utapitia miradi Miradi 13 yenye thamani ya sh. shilingi bilioni 10.5.
Miongoni mwa miradi iliyopitiwa na mwenge wa uhuru ni pamoja na ujenzi wa madarasa mawili na ofisi moja katika shule ya msingi Uhuru, mradi wa vijana wa ufugaji kuku, uzinduzi wa huduma za upasuaji katika hospitali ya wilaya pamoja na ukaguzi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya amali iliyoko katika kijiji cha Minazimikinda
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.