Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2019, Mzee Mkongea Alli amewataka watendaji wote chini kuacha mara moja tabia ya kuhujumu ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo miradi yan maji huku akielekeza kuwa mtendaji atakaebainika kushiriki katika hujuma hizo achukuliwe hatua kali za kisheria.
Akizungumza katika makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru katika kijiji cha Kipara Mpakani, Mkuranga mkoani Pwani , ukitokea Mkoani Dar es salaam ,Ali alisema haiwezekani serikali itekeleze mipango mizuri ili kuboresha sekta ya maji kisha atokee mtendaji wa chini kukwamisha juhudi hizo.
“Washukieni wazimawazima, Rais dk.John Magufuli alivyoingia madarakani aliahidi kutekeleza kuboresha sekta hiyo na kuleta maendeleo,na ana fanyakazi nzuri sasa watendaji wa chini wanaosuasua wana maana gani!!tushirikiane kuonyesha jitihada zinazofanywa na serikali”alieleza Ali.
Alielezea kuwa maji ni haki ya kila mtu, hivyo vyanzo vya maji vitunzwe kwa maslahi ya jamii.
Pia kiongozi huyo za mwenge,aliwataka wananchi kushiriki katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na vitongoji.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo akipokea mwenge wa Uhuru alisema kuwa Mwenge wa Uhuru ukiwa mkoani hapa utakimbizwa kwenye Wilaya saba na ,halmashauri Tisa ambapo miradi 95 itapitiwa yenye thamani ya sh.Bilioni 40.436.6, kati ya miradi hiyo miradi 61 itakaguliwa,17 itawekwa jiwe la msingi,9 itazinduliwa na 8 itafunguliwa
.
Akizungumzia sekta ya maji, mhandisi Ndikilo alibainisha kuwa asilimia 52 ya watu mkoani humo wanapata huduma ya maji safi na salama na wanaopata maji watu 790,000 sawa na asilimia 67 ya wakazi wote milioni 1.2.
Wakati huo huo ,mkuu wa wilaya ya Mkuranga Filberto Sanga alisema ,mwenge huo utatembelea miradi nane yenye thamani ya bilioni 5.177.
Mwenge wa Uhuru upo mkoani Pwani ukiwa ni mkoa wa 21 tangu ulipozinduliwa mkoani Njombe
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.