Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa 2019 ,Mzee Mkongea Ali amemuagiza kamanda wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Rufiji kuchunguza ubadhilifu wa fedha uliotokea katika mradi wa maji Ikwiriri uliojengwa na mamlaka ya maji safi Dar es salaam DAWASA kwa gharama ya sh.bilioni 2.055.648.243.
Ametoa agizo hilo wakati mwenge wa uhuru ulipotembelea mradi huo na kubaini baadhi ya dosari na kukosa nyaraka muhimu zilizotumika katika manunuzi ya baadhi ya vifaa.
Amemtaka kamanda wa TAKUKURU ndani ya wiki mbili kukamilisha agizo hilo kisha kupeleka taarifa TAKUKURU makao makuu na nakala itumwe kwake ili kama kutabainika uchakachuaji hatua ziweze kuchukuliwa.
Nae mkuu wa wilaya ya Rufiji, Juma Njwayo amemwakikishia kiongozi huyo wa mbio za mwenge kuwa atalisimamia suala hilo kwakuwa kabla ya mwenge kuanza ziara hiyo viongozi wa wilaya hiyo walishiriki kikao cha kamati ya sherehe ambacho kiliitishwa na mkuu wa mkoa na kuagiza kwamba wataalamu kutoka Dawasa kuwepo katika miradi yote ya maji itakayopitiwa na mwenge lakini cha ajabu katika mradi huo hawajafika katika wilaya hiyo.
Njwayo alisema, mwenge wa uhuru ukiwa wilayani Rufiji umepitia Tisa yenye thamani ya sh.bilioni 2.562 .
Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa maji shule ya msingi Umwe,mradi wa maji Ikwiriri,kikundi cha vijana Mkongoni cha uselemala,ukarabati wa kituo cha afya Ikwiriri,ukarabati wa chuo cha maendeleo ya wananchi Ikwiriri ,mradi wa nyumba za kulala wageni Mloka safari lodge na kikundi cha walemavu Mloka.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.