KATIKA kuunga mkono azma ya Rais wa awamu ya tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na uchumi wa viwanda serikali Mkoa wa Pwani imejipanga mwezi huu kuweka mawe ya msingi katika viwanda vipatavyo 13 ambavyo vitajengwa katika Wilaya za Kibaha, Bagamoyo, pamoja na Mkuranga kwa lengo la kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake wakiwemo baaadhi ya wakuu wa idara Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bi Theresia Mmbando amebainisha kuwa zoezi hillo la kuweka mawe ya msingi na kukagua ujenzi wa viwanda hivyo litafanywa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndaikilo ikiwa ni moja ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Aidha katika hatua nyingine amekemea vitendo vya baadhi ya wawekezaji kuwanyanyaza wafanyakazi ambao ni wazawa na badala yake kuwataka kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote za kazi na kuwapa vipaumbele zaidi wananchi katika fursa za ajira ili kutimiza malengo ya serikali katika kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda.
Mkoa wa Pwani katika zoezi hilo litaweka mawe ya msingi katika baadhi ya viwanda hivyo vikiwemo vya kiwanda cha kutengenezea mikate na biskuti, kiwanda cha kuzalishia nyuzi, kutengenezea nondo, sufuria, mitungi ya gesi, kiwanda cha kuchakata mihogo, kamba za uvuvi pamoja na kingine cha kuchakata zao la korosho pamona na kinachozalisha chanjo za mifugo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.