• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

Ndikilo aelekeza Usajili wa watoto chini ya Miaka Mitano kuvuka asilimia 90

Posted on: November 27th, 2019

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo ametoa maelekezo kwa viongozi mkoani hapa kuhakikisha kuwa usajili na utoaji wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto walio chini ya miaka mitano unafikia Zaidi ya asilimia 90 ndani ya miezi mitatu kuanzia sasa.

Akifungua semina kwa viongozi wa Mkoa na wilaya juu ya Mpango wa usajili wa watoto walio na umri chini ya miaka mitano iliyofanyika Wilayani Mkuranga, Mhandisi Ndikilo alisema kuwa takwimu zinaonesha kuwa kwa sasa waliosajiliwa na kupewa vyeti vya kuzaliwa mkoani Pwani ni asilimia 14.5 tu, hivyo akawaeleza viongozi hao kuwa wanao wajibu wa kuhakikisha kuwa zoezi hilo linaratibiwa vizuri ili kufikia lengo la kusajili na kutoa vyeti kwa watoto wote walio na vigezo.

Akifafanua jukumu la kila mdau, Mhandisi Ndikilo aliwaasa wakurugenzi na timu zao kwenda kutekeleza kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya kutoshakuhusu jambo hili na wakuu wa wilaya kufanya ufuatiliaji wa karibu.

“Halmashauri wanapewa fedha za utekelezaji wa mpango huu, ninawaasa zikatumike kwa matumizi yaliyokusudiwa na si vinginevyo, madiwani wasiwakomalie wakurugenzi kutumia fedha hizo, kazitumieni vizuri ili mfanye kazi hii sawasawa, msije mkaiona fedha hiyo kuwa ni yenu” alisisitiza Mhandisi Ndikilo.

Mhandisi Ndikilo alieleza kuwa Mpango huu utasaidi kuondoa tatizo la kuchelewa kwa upatikanaji wa Vyeti vya kuzaliwa kwa Wananchi wa Mkoa Pwani kwa kuwa limepatiwa suluhisho la kudumu na akatahadharisha kuwa wasajili katika vituo waondoe urasimu wakati wa usajili na kutoa vyeti kwani huduma hiyo inatekelezwa bila malipo yoyote kutoka kwa mzazi au mlezi wa mtoto husika, hivyo wasiitumie kama moja ya njia ya kujipatia kipato.

Kuhusu umuhimu wav yeti vya kuzaliwa, Mhandisi Ndikilo aliesma kuwa kinasaidia kuwapata viongozi wazawa, kinasaidia kwa mipango ya taifa, masuala ya ulinzi, kusaidia upatikanaji wa hati za kusafiria nje ya nchi, upatikanaji wa ajira, upatikanaji wa mafao pale ajira inapokoma na hata kuwarahisishia viongozi wa Dini mbalimbali kutekeza majuku yao wakati wakitoa huduma kwa washiriki kama vile za ndoa.

Awali katika katika taarifa yake Kaimu  Afisa Mtendaji wa RITA Bi. Emmy Hudson alieleza kuwa hadi sasa kupitia mpango huo utekelezaji katika mikoa 15 umesaidia kuwapatia hati watoto bila kujali hali zao na kupandisha takwimu kutoka asilimia 13 mwaka 2012 hadi 49 mwaka 2019.

Bi. Hudson aliongeza kuwa miongoni mwa mambo mengine, Mpango huo umesaidi pia upatikanaji wa (papo kwa hapo) haraka wa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto wanaozaliwa pamoja na upatikanaji wa takwimu zilizo sahihi.

                                            

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RS Pwani Yaibuka Kidedea kwa Ushindi wa "-1 Dhidi ya Kibaha TC

    May 01, 2025
  • Rais Samia Apongezwa kwa kuwa Kiongozi wa Mfano katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mkoani Pwani

    May 01, 2025
  • RC Kunenge Aagiza CORECU Kutekeleza Maomo ya Rais Samia Kuhusub Ushirika

    April 30, 2025
  • Spika Tulia Asisitiza Umuhimu wa Muungano katika kuimarisha Umoja na Amani

    April 25, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.