Muu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo ametoa rai kwa waumini wa dini ya Kiislam wakati wakiendelea na mfungo wa mwezi wa Ramadhani kutumia muda kuliombea Taifa kuendelee kuwa tulivu, kumuombea Rais mama Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake wakatekeleze majukumu yao kama walivyopanga.
Ndikilo alitoa rai hiyo katika hafla fupi ya futari aliyoiandaa kwa ajili ya watu mbalimbali wa mkoa huo kushiriki futari pamoja nyumbani kwake.
Ndikilo alitumia nafasi hiyo kuwasihi waumini wa dini hiyo kutumia muda wa mfungo kuliombea Taifa na kila Jambo lililopangwa na Rais na wasaidizi wake lifanyike kwa ufulivu.
Aidha alitoa rai kwa viongozi wa Halmashauri kuhakikisha fedha zinazopitishwa kwenye bajeti na kufika kwenye maeneo yao zinasimamiwa vizuri.
Alisema tayari bajeti ya zaidi ya shilingi bilion mbili ya mkoa huo imeshapitishwa Bunngeni hivyo ni vema zitumike kama zilivyolengwa na Halmashauri zisiangukie katika hati chafu
Aliwataka viongozi ngazi ya Wilaya kuendelea kuwapa ushirikiano wawekezaji wanaofika kwenye maeneo yao ili wapate huduma zote zinazotakiwa kwa wakati.
Akizungumzia katika suala la Elimu alisema Mkoa huo umejipanga kuinua kiwango cha ufaulu kwa wahitimu kuanzia ngazi ya msingi na kuendelea kushika namba nzuri kitaifa.
Ndikilo alisisitiza suala la wenye dhamana ya kutoa haki kuendea kiufanya hivyo kwa wananchi hususani wanyonge.
Aliwakumbusha wakazi wa mkoa huo kuendelea kukata bima ya afya ili kuondoa usumbufu na malipo ya gharama kubwa pindi wanapoumwa.
" Hadi sasa ni asilimia 5.1 ya wakazi wa mkoa huu ambao Wana bima ya afya, tambueni kuna faida ya kukata bima kwa familia magon wa hayapigi hodi na hujui yatakukuta ukiwa na hali gani" alisema
Katika neno lake la shukrani kwa waliohudhuria kwenye futari hiyo aliwasihi wafanyabiashara kuwasaidia waumini was dini ya Kiislam kwa kuwarahisishia upatikanaji wa bidhaa wanazobitaji kwa ajili ya futari kwa gharama ileile na kuepuka kutumia kipindi hkii kujinufaisha.
Mkuu wa mkoa alitoa futari kwa vituo vitano vya kulelea watoto yatima iliyogharimu kiasi cha Shilingi Milion mbili
Akishukuru baada ya hafla hiyo Shekhe mkuu wa mkoa wa Pwani Hamis Mtupa alimpongeza mkuu huyo wa mkoa kwa kuwakumbuka waumini wa dini ya Kiislam na majirani zake na kufuturu nao pamoja kwani kwa njia hiyo inamuweka karibu na Mungu.
Alionya baadhi ya watu ambao wanatumia vituo vya watoto yatima kujinufaisha huku akisisitiza kila mmoja kuwaonea huruma watoto yatima.
“hgyuhjhbhju Kama kuna mtu anamkashifu Mungu asiachwe kwani kwa kipindi tulichonacho tuendelee kuwa karibu na Mungu"
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.