Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo, ameutaka uongozi wa DAWASA Mkoani Pwani kuhakikisha wanawasimamia vizuri wakandarasi waliopewa kutekeleza mradi wa usambazaji maji katika maeneo ya EPZDA na maeneo mengine na kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati.
Rai hiyo aliitoa mwishoni mwa wiki hii ,wakati alipokuwa katika ziara yake ya kukagua na kuangalia miradi ya DAWASA inavyoendelea kutekelezwa Wilayani Bagamoyo.
Katika Hatua nyingine Mhe. Ndikilo, amepongeza hatua iliyofikiwa ya utandikaji wa mabomba na ujenzi wa tanki kubwa ambalo litakuwa na uwezo wa kuhifadhi maji lita million 6 kwa wakati mmoja.
Aidha amekemea vikali tabia ya wananchi kufanya shughuli za kibinadamu pembezoni mwa mto Ruvu, na kuwataka waache mara moja tabia hiyo.
“Sintasita kumchukulia hatua kali za kisheria kwa mtu yeyote yule atakayeendelea kufanya shughuli za kibinadamu kando kando ya mto Ruvu alisema Mkuu wa mkoa Mhe. Engr Ndikilo.
Pia alisema kuwa mto Ruvu hutegemewa kwa asilimia 88% kwa uzalisha maji yanayotegemewa na Wakazi wa Mkoa wa Pwani na Dar es salaam.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.