MKoa wa Pwani ,umepiga hatua kali na kufikia kuwa na viwanda vikubwa,vya kati,vidogo na vidogodogo 1,236 kwa mwaka 2020 kutoka viwanda 396 kwa mwaka 2016.
Kasi hiyo ya ujenzi wa viwanda ni kubwa ndani ya miaka minne ,ambapo viongozi watendaji wa mkoa huo wameamua kuongeza jitihada za kuhamasisha wawekezaji ili kuhakikisha mkoa huo unakuwa Ukanda wa Viwanda.
Akielezea mafanikio hayo ,Mkuu wa mkoa wa Pwani, mhandisi Evarist Ndikilo alisema ,bado wamejipanga kuongeza viwanda na wawekezaji ili kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Pamoja na hayo ,alieleza kati ya wilaya zote mkoani hapo ,lakini bado wilaya tatu ya Kibiti,Rufiji na Mafia zinasuasua kufikia kasi hiyo .
Kutokana na hilo ,ameelekeza nguvu ielekezwe katika wilaya hizo kwani fursa zipo .
"Tunapokea pongezi na sifa nyingi kutoka kwa viongozi wakuu Taifa akiwemo Rais John Magufuli ,mikoani na nchi mbalimbali hivyo nawataka viongozi mkoa kuendelea kulinda maendeleo hayo na kuinua sekta ya viwanda" alibainisha Ndikilo.
Akielezea juu ya sekta ya elimu ,ameelekeza kuhakikisha madarasa yanayopaswa kujengwa yajengwe ,ili wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza January 2021 wawe wote darasani ,kwani bado wanafunzi 6,577 wanaonekana watakosa kuingia madarasani.
Akizungumzia tatizo la upungufu wa watumishi , alisema pamoja na juhudi za mkoa lakini changamoto hii inajirudia kila mwaka.
Katibu tawala msaidizi mipango na uratibu Edward Mwakipesile alifafanua ,kuna changamoto kubwa ya upungufu wa watumishi mbalimbali na idara ya afya upande wa wataalamu wa Xray ni shida .
Nae mkuu wa wilaya wa Mafia , Shaibu Nnduma alisema ,idara 14 zinakaimisha watendaji na wote wanaokaimu hawana sifa.
Kufuatia changamoto hiyo ,katibu mkuu TAMISEMI alifikishiwa taarifa hizo na kuomba tena awasilishiwe juu ya hilo na kuhusiana na tatizo la Mafia amedai atafika mwenyewe Mafia .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.