Zaidi ya sh. trilioni moja zimetolewa na serikali katika kipindi cha miaka miwili kwa ajili ya kuteleza miradi mbalimbali ya mendeleo ikiwemo sekta ya afya, umeme, elimu na miondombinu kama vile barabara.
Hayo yamesemwa Agosti 27, 2023 na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge wakati wa kufunga mafunzo ya Uongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala Tanzania bara ambayo yalianza Agosti 22 hadi 27 katika Ukumbi wa Chuo cha Uongozi kilichopo Halmashauri ya Mji wa Kibaha mkoani Pwani.
Amesema katika kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wamepatiwa kiasi cha sh trilion 1.1 ambapo kati ya fedha hizo sh milioni 506 kwa ajili ya kukamilisha miradi ya umeme, milioni 102 kwa ajili ya ujenzi wa barabara, Afya bilioni 19.5 na elimu bilioni 92.8.
“Tunakushukuru Rais wetu mpendwa kwa kutupatia fedha nyingi kutekeleza miradi ya maendeleo katika kipindi cha miaka miwili, aidha tunajivunia kuona mkoa wetu unamiliki viwanda vingi vikiwemo vikubwa vya kati na vidogo,”amesema Kunenge.
Amefafanua kuwa kwa sasa mkoa wa Pwani una viwanda 1522 ambapo kati yao vikubwa ni 117 na vya kati 120 na kwamba kwa kipindi cha miaka miwili jumla ya viwanda vikubwa 22 vilifunguliwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.