Mkoa wa Pwani umeweza kupunguza vifo vya mama wajawazito kutoka vifo 37 na kufikia vifo 12 na watoto toka vifo 358 hadi 178 kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kuanzishwa mfumo wa Rufaa unaotembea wa (M-MAMA).
Hayo yalisemwa Mjini Kibaha na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani David Vuo wakati wa mafunzo kwa maofisa habari na waelimisha umma wa mkoa wa Pwani juu ya mfumo huo.
Vuo alisema kuwa mfumo huo kwa Mkoa ulizinduliwa mwaka 2023 umeleta mafanikio hayo ambayo ni makubwa kwani malengo ni kupunguza vifo vya akinamama na watoto ikiwa ni mikakati ya kuboresha huduma za afya ya uzazi na mtoto.
"Katika kipindi hicho cha mwaka mmoja mfumo umeweza kuwasafirisha mama wajawazito zaidi ya 2,000 kwa kutumia madereva ambao wameingizwa kwenye mfumo huo wa magari ya kusafirisha wagonjwa ngazi ya jamii,"alisema Vuo.
Kwa upande wake mratibu wa mpango huo kwa Mkoa Alfred Ngowi alisema kuwa waelimishaji ngazi ya jamii sasa wataenda ngazi ya vijiji na wahudumu wanachaguliwa toka sehemu wanayoishi ili waweze kuwaibua na kuwaunganisha na mfumo huo.
Ngowi alisema jamii itarajie huduma ya dharura inakwenda kuwafikia mama yoyote mjamzito au mtoto toka siku moja hadi siku 28 ataunganishwa na dereva ngazi ya jamii na kupelekwa ngazi kituo cha afya kupata huduma.
Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo Gabriel Mtwale jamii itapiga simu ili wapate huduma mzazi anatoka nyumbani kwenda kwenye kituo cha huduma ambapo kulikuwa na changamoto kama hana fedha za kusafirishwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.