Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge ameeleza Nia ya Mkoa huo ni kuendelea kufungua mtandao wa miundombinu bora ya barabara inayoakisiana na kasi ya uwekezaji iliyopo Mkoani humo.
Aidha ameeleza, nia ya mafanikio hayo itawezekana endapo kutakuwa na mazingira wezeshi ikiwemo kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji na migogoro ya ardhi.
Akifungua , kikao cha bodi ya barabara Januari 4, 2023, kilichofanyika mjini Kibaha na kuhudhuriwa na wajumbe kutoka katika wilaya mbalimbali za mkoa wa Pwani, Kunenge alieleza kuwa , mtandao wa miundombinu bora unatoa fursa kwa wawekezaji ,kurahisisha usafiri kwa jamii na kufungua mkoa kiuchumi .
Hata hivyo, alisema Mazingira wezeshi yakiimarika na kupunguza migogoro ya ardhi itaisaidia kuinua maendeleo na mkoa kuendelea kuwa kimbilio la wawekezaji.
" Tumechoka migogoro ya wakulima na wafugaji hili ni jambo ambalo kama hatutaliondoa vikwazo vitaendelea kubaki pale pale," Tumeona dhamira ya Rais wetu kufungua mkoa wetu ,hivyo ni wajibu wetu sisi kuangalia barabara zenye tija ,tuangalie mkoa wetu kwa ujumla wake ,tunajua nchi yetu ina vipaombele vingi, lazima tupendekeze miradi yenye hoja ,na inayokubalika yenye kuwagusa wananchi na tija kiuchumi,"
"Tunatakiwa tuwe na hoja inaringanishwa na mikoa mingine, barabara zinasaidia kugusa maisha ya wananchi na kukuza uchumi Lakini ukipata barabara inayogusa wananchi na uchumi inakuwa na tija zaidi "alifafanua Kunenge.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.