Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe Mhandisi Evarist Ndikilo amefungua Warsha ya siku moja ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Serikali na Sekta Binafsi Mkoani hapo juu ya dhana ya Kongano.
Ndikilo ameipongeza SIDO kwa kuendesha Warsha hiyo yenye lengo la Kujenga uelewa wa pamoja wa dhana ya Kongano, akizungumzia Dhana ya Kongano Ndikilo amesema; Dhana ya Kongano ni kutambua faida za kiushindani kwa kuwezesha na kuimarisha uunganishwaji na ushirikiano baina ya wadau mbalimbali.Ameeleza Kongano ni mkusanyiko wa Viwanda vilivyo karibu karibu vinavyofanya shughuli zinazo fanana zikisaidiwa na watoa huduma, ametaja faida za Kongano hizo ni pamoja na kuwezesha wajasiriamali hao kupata Mikopo, Teknolojia, taarifa za masoko na huduma za taasisi kama vile TBS, TFDA n.k.
Akizungumza kwenye Warsha hiyo Ndikilo amewataka washiriki wa Warsha hiyo, kuandaa Mpango wa Ujenzi wa Viwanda kwa maeneo yaliyotengwa kwa Ujenzi wa Viwanda, kuchagua mazao ya Kimakakati ya kuanzisha Kongano, ametolea mfano wa Zao la Nazi na Mwani kwa Wilaya za Mafia, Mhogo kwa Wilaya za Kibiti na Mkuranga, Matunda kwa Wilaya za Bagamoyo na Chalinze. "
"Katibu Tawala Mkoa Tuwapelekee maelekezo mahususi Halamshauri zetu Kuhusu uanzishwaji wa Kongano na kuwasimamia katika Kuanzisha na kuchagua mazao ambayo yatamkomboa Mkulima, amewataka Maafisa Mipango wa Halmshauri Mkoani humo kuandaa mipango kazi ya Utekelezaji wa dhana Kongano na kuingiza kwenye Bajeti za Halmshauri. Nataka Mkoa wetu utoke kwenye ordha ya Mikoa ambayo hazijaanzisha Kongano.
Ndikilo amesema nafasi ya Mkoa huo na Wilaya katika Kuendeleza Viwanda ni pamoja na kuwezesha uanzishaji wa Kongano hizo, amewataka SIDO Mkoa wa Pwani kuhakisha wanalisimamia ili litekelezwe kwa haraka ndani ya kipindi kifupi. Amesema jukumu jingine ni kuandaa Mwongozo wa Uwekezaji Mkoa ambao tayari umeandaliwa na ulizinduliwa mwaka 2019, kufanya maonesho ya Viwanda, kutembelea Miradi ya Sekta Binafsi, kufanya vikao vya Mabaraza ya biashara Mkoa, Uanzishwaji wa madawati ya Uwekezaji na Viwanda."Mambo haya yamelenga Kuanzisha na kuendeleza Viwanda kwenye Mkoa wetu" alisema Ndikilo.
Akitaja mafanikio ya Sekta ya Viwanda Ndikilo amesema Mkoa huo una viwanda 1236 vikubwa 68, vya Kati, 112, Vidogo 168 na Vidogo sana 888
Ameeleza Siri ya kupiga hatua kubwa kwenye Ujenzi wa sekta ya Viwanda ni pamoja na Viongozi kuanzia ngazi ya kitongoji hadi Mkoa kuzungumza lugha moja kuhusiana na Uwekezaji, Kuondoa urasimu katika kuhudumia wawekezaji na kutatua changamoto za wawekezaji kwa kuwaunganisha na Taasisi Wezeshi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.