Mkoa wa Pwani umeungana na Watanzania wengine kuadhimisha siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendesha zoezi la upandaji wa miti 6,379 kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais katika kulinda na kutunza mazingira.
Akizungumza na waandishi wa habari Januari 26, 2026, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Abubakar Kunenge, amesema zoezi hilo litafanyika tarehe 27 Januari 2026 na litahusisha upandaji wa miti ya matunda 671 pamoja na miti 5,708 ya mbao na vivuli, ambayo itapandwa katika maeneo ya shule ili kuwajengea wanafunzi utamaduni wa kutunza mazingira.
Aidha, Mhe. Kunenge ameeleza kuwa zoezi hilo ni sehemu ya mpango wa Mkoa wa Pwani wa kupanda jumla ya miti 13,500,000 wakati wa mvua za masika, sambamba na ugawaji wa miche ya mikorosho 1,500,000 kwa wakulima wa Wilaya ya Rufiji, chini ya kauli mbiu “Uzalendo ni Kutunza Mazingira – Shiriki Kupanda Miti.”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.