Mkoa wa Pwani umeandaa maonesho ya nne ya Biashara, Uwekezaji na Pwani Konekt kwa lengo la kuongeza uwekezaji, kukuza biashara, na kuendeleza fursa za maendeleo endelevu katika uchumi wa bluu na kidijitali.
Katibu tawala msaidizi Viwanda, Biashara na Uwekezaji Rehema Akida amesema kuwa maonesho hayo yanatarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 10 hadi 16 Desemba mwaka huu katika viwanja vya Stendi ya Zamani ya Mabasi Maili Moja, wilayani Kibaha, Mkoani Pwani.
Ameeleza kuwa maonesho hayo yatawezakuwakutanisha wafanyabiashara wakubwa, wa kati, na Wadogo kutoka ndani na nje ya Tanzania kwa ajili ya kuchangamkia fursa za uwekezaji na biashara katika Mkoa wa Pwani na kukuza soko la bidhaa za Tanzania.
Pamoja na maonesho, ameeleza kutakuwa na kongamano la Uwekezaji litakalofanyika tarehe 12 Disemba 2024 katika ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere, Kibaha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.