Bidhaa mbalimbali zinazozalishwa kwenye viwanda vilivyoko mkoani Pwani zimeendelea kuitambulisha Tanzania nje ya nchi kutokana na ubora wake.
Hayo yamesemwa leo Oktoba 20, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan alipokuwa akihutubia wananchi wa Wilaya ya Mkuranga katika Viwanja vya Mwandege, mkoani Pwani.
Akitolea mfano Dkt. Samia amesema kuwa bidhaa za vioo vinavyozalishwa Mkoani humo vimepata soko kubwa katika nchi za jirani.
Amesema mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa sera bora za Serikali katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji nchini.
Aidha, amepongeza juhudi za wananchi na viongozi wa Mkoa wa Pwani kwa kuunga mkono jitihada za Serikali katika kukuza sekta ya viwanda, na kusisitiza kuwa Mkoa huo unaendelea kuwa kitovu cha maendeleo ya viwanda nchini na kuahidi kujenga kongani za Viwanda katika kila wilaya za Mkoa huo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.