Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, amesema kuwa Mkoa wa Pwani umeunda kamati mbalimbali kwa ajili ya tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona katika Halmashauri zote tisa.
Hayo amebainisha wakati akifungua kikao Maalumu cha dharura Cha Afya ya msingi, kilichofanyika machi 20, kikiwa na lengo la kuweka mikakati ikiwa atapatikana mgonjwa wa Corona kwa Mkoa hapa
Mhandisi Ndikilo alisema, kamati hizo zitakuwa na majukumu ya Kupambana na kudhibiti ugonjwa huo katika nyanja zote.
Aidha alisema kuwa katika Mkoa huo watu wanne walishukiwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo , ambao walipochukuliwa sampuli majibu yote yalionyesha hawana maambukizi.
Mhandisi Ndikilo alisema, wananchi wakaendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na ugonjwa huo kwa kufuata miongozo mbalimbali inayotolewa na idara ya Afya ba Serikali kwenye maeneo yote.
" Sisi kama Mkoa tutasimamia maagizo yanayotolewa, ili kuhakikisha kuwa jamii yetu ya Mkoa wa Pwani inaendelea kuwa salama na bila kuwa na ugonjwa huu" alisema Mhandisi Ndikilo.
Katika Hatua nyingine Mhandisi Ndikilo kwa viongozi wa ngazi zote kuhakikisha kuwa mipango kwa ajili ya Kupambana kudhibiti ugonjwa huo iliyoandaliwa inatekelezwa kikamilifu.
Wakati huo huo alitoa agizo kwa mamlaka ya maji safi na maji taka (DAWASA) kuhakikisha maji hayakatiki ili wananchi watumie kunawa mikono Mara kwa Mara kwa kutumia sabuni.
Nae Mganga mkuu wa Mkoa wa Pwani Dkt Gunini Kamba alisema kuwa kuhusiana na vitakasa mikono , wananchi watatangaziwa sehemu ya kuzipata kwa gharama nafuu, na kwasasa utaratibu unaendelea kwa kuwasiliana na bohari ya madawati kufungua duka litakalopunguza adha ya kupatikana dawa hizo.
Mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogowadogo (Machinga) Philemon Maliga aliomba elimu zaidi itolewe kwa kundi hilo ambalo linazunguka katika minada mbalimbali ya biashara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.