Jumla ya watoto wachanga 475 wamefariki dunia baada ya akinamama 41,064 kujifungua Mkoani Pwani mwaka 2018 , hali ambayo inaonyesha idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi kimkoa kuwa juu.
Aidha kati ya akinamama hao 41, 064 waliojifungua akinamama 67 walifariki dunia kutokana na uzazi.
Hayo yalielezwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,dokta Gunini Kamba , wakati Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Mhandisi Evarist Ndikilo aliposaini hati ya makubaliano na wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Pwani juu ya kampeni ya kuzuia vifo vinavyotokana na uzazi, kampeni ambayo itafanyika kwa muda wa miezi 12
Dokta Kamba alisema kuwa vifo vya watoto wachanga na akinamama wanaojifungua vimekuwa vingi hali ambayo hairidhish,i hivyo kampeni hiyo itasaidia kupunguza idadi ya vifo hivyo
“Lengo hilo linaweza kufikiwa endapo akina mama watafuata maelekezo ya kiafya wanayopatiwa wakati wa uzazi ili waweze kuvuka salama katika kipidi cha uzazi “alisema Dkt Kamaba.
Pamoja na hayo Dkt Kamba aliwataka akinamama wajawazito kuhakikisha kuwa wanaanza kliniki mapema pindi wanapoona dalili za ujauzito ili kujua afya zao.
Pia waendelee kufatilia afya zao kulingana na utaratibu watakaopatiwa hadi wakati wa kujifungua bila kupuuzia.
“Na wakijifungua inapaswa kuhakikishiwa ndani ya lisaa limoja baada ya kujifungua mtoto anyonye “alifafanua Dkt kamba.
Akihitisha zoezi hilo nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani , Mhandisi Evarist Ndikilo aliwataka Wakuu wa Wilaya kwenda kusimamia malengo hayo ili kufanikisha kampeni hiyo kiwilaya , kimkoa na kitaifa kwa kiujumla.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.