Mkoa wa Pwani umetenga maeneo 27 kwa ajili Kongani mchanganyiko, maalum na za kibiashara ili kukuza Uwekezaji.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge leo Septemba 11, 2025 ofisini kwake alipokutana na kufanya mazungumzo na sehemu ya Menejimenti ya Taasisi ya Uhandisi na Usanifu Mitambo Tanzania - TEMDO uliyoongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Eng. Prof. Frederick Kahimba.
Kunenge alieleza kuwa uwepo wa fursa za Uwekezaji zimefanikisha ongezeko la Viwanda kutoka 1387 Mwaka 2021/2022 kufikia 1631 Mwezi Juni 2025 sawa na ongezeko la asilimia 18.
Kwa upande wake Eng. Prof. Kahimba alisema wameandaa mkakati wa kuanzisha utengenezaji wa vipuri na mitambo yenye ubora na ufanisi katika kuchakata malighafi na kuzalisha bidhaa ambavyo watu wenye mitaji midogo wanaweza kumudu gharama zake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.