Jumla ya nyumba 515,668 zimeingizwa kwenye mfumo wa Zoezi la anwani za makazi sawa na asilimia 105.61 Mkoani Pwani.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge alipotoa taarifa ya Mkoa Kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru za Mwaka 2022.
Katika mapokezi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru za Mwaka 2022 ambayo yamefanyika katika Kijiji cha Kiwanga Wilayani Rufiji kutoka Mkoa wa Lindi leo Mei 1, 2022, Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge alisema kufuatia maandalizi ya sensa na makazi Mkoa wa Pwani umejipanga na kuendelea kuhimiza wananchi kujitokeza kwenye Zoezi hilo litakalotekelezwa mwezi Agost mwaka huu.
"Mkoa wetu ni miongoni mwa mikoa 13 iliyoshiriki kwenye zoezi la sensa ya majaribio na Tunashukuru tumefanya vizuri " Kunenge alisema.
Mkuu huyo wa mkoa alieleza kuwa,kiasi cha sh.milioni 816 .2 kutoka Serikali Kuu kimepokelewa na Halmashauri zimechangia milioni 320.
Pamoja na hayo, Kunenge alieleza mwenge wa uhuru ukiwa Mkoani hapo utapitia miradi 111 yenye gharama ya Zaidi ya Bilioni 69.2.
"Kati ya miradi hiyo miradi 25 itawekwa mawe ya msingi, 22 itazinduliwa,6 itafunguliwa na 58 kukaguliwa"alifafanua Kunenge.
Akipokea mwenge wa uhuru Mkuu wa wilaya ya Rufiji Edward Gowelle kutoka kwa Mkuu wa mkoa,alisema mwenge ukiwa Rufiji utapitia miradi sita yenye thamani ya milioni 600.5.
Kati ya miradi iliyotembelewa Rufiji ni pamoja na Zahanati Nyanda Katundu, barabara Mji Utete, mradi wa vijana kikundi cha Kumekucha Umwe Kaskazini, Mradi wa Uraghibishaji falsafa ya mwenge,ghala la mwananchi na madarasa ya Sekondari Mkongo.
Mwenge wa uhuru Mei 2 unatarajiwa kupokelewa huko Mkupuka wilaya ya Kibiti.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.