Kamati ya Amani ya Mkoa wa Pwani imetembelea eneo la Mradi wa Umeme wa mto Rufiji na kufanya maombi maalum ili utekelezaji wake ukamilike kwa ufanisi na kwa wakati uliopangwa.
Kamati hiyo yenye wajumbe kutoka madhehebu mbalimbali imeshiriki kwenye ziara ya siku tatu iliyoanza April tisa ikijumuisha Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Pwani na ya Wilaya ya Rufiji, Wakuu wa Wilaya sita, Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji pamoja na Viongozi wa Serikali ya Kijiji cha Mloka.
Wakiwa katika eneo la mradi, msafara huo ulioongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo ulipokea maelezo ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa kimkakati kutoka kwa Wataalamu wa Shirika la Umeme nchini-TANESCO wanaosimamia mradi huo.
Akifafanua lengo la ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Mhandisi Evarist Ndikilo alieleza kuwa sehemu ya eneo la ujenzi wa mradi liko katika Mkoa wa Pwani hivyo ni wajibu wa jamii kuwa na uelewa mpana na wajibu wa kushiriki katika utekelezaji na kulinda miundombinu yake ikiwa ni pamoja na kubaini changamoto zilizopo au zinazoweza kujitokeza na kuzipatia ufumbuzi.
“Asilimia kubwa ya shughuli za utekelezaji wa mradi huu zitakuwa katika eneo la Mkoa wa Pwani hivyo tunataka tuone namna ambavyo Kamati ya Ulinzi na Usalama na Kamati ya Amami itashughulikia maswala yote yaliyoko ili mradi huu usikwame” amesema Mhandisi Ndikilo.
Mkuu wa Mkoa ameongeza kuwa pamoja na kuwa wataalamu wa kitanzania na Mkandarasi wako kwenye eneo la utekelezaji wakiendelea na majukumu yao, bado kuna mambo mengine nje ya eneo hilo ambayo Mkoa kwa kushirikiana na Taasisi nyingine zinawajibu wa kuyasimamia ili kuhakikisha kuwa utekelezaji unafanikiwa na kwa wakati.
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Bibi. Theresia Mmbando (aliyeshika mic) akitambulisha msafara wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na ile ya Amani zote za Mkoa wa Pwani mara baada ya kufika kwenye eneo la Mradi wa Umeme wa mto Rufiji
Mhandisi Joseph Kiyumbi wa TANESCO (wa kwanza mbele aliyevaa shati jeupe) akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na kamati ya Amani Mkoa wa Pwani
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akifafanua Mkakati wa Mkoa katika kufanikisha utekelezaji wa Mradi wa Umeme wa mto Rufiji wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na kamati ya Amani Mkoa zilizotembelea eneo la mradi huo.
Mhandisi Joseph Kiyumbi wa TANESCO (aliyevaa kofia nyeupe) akitoa maelezo ya utekelezaji wa Mradi kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na kamati ya Amani Mkoa wa Pwani
Mhandisi Joseph Kiyumbi wa TANESCO (wa pili toka kushoto) akimuogoza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza toka kulia) na msafara wake kutembelea eneo la utekelezaji wa Mradi
Mhandisi Mwanji Yohana wa TANESCO (mwenye kofia Nyeupe) akimuogoza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (mwenye karatasi mkononi) na msafara wake kutembelea eneo la utekelezaji wa Mradi
Msafara ukiwa katika moja ya maeneo ya utekelezaji Mradi
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (wa Pili toka kushoto mbele) akifuatilia maelezo ya Mradi toka kwa Mhandisi Joseph Kiyumbi wa TANESCO (aliyevaa kofia nyeupe)
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo (wa Pili toka kushoto mbele) akielekeza jambo kwa Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na kamati ya Amani Mkoa wa Pwani
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.