Mkoa wa Pwani, umeongoza kwa idadi kubwa ya shule za Sekondari na watahiniwa kwenye orodha ya kumi bora kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018.
Kufatia matokeo yaliyotangazwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dkt Charles Msonde katika orodha ya shul ezenye watahiniwa zaid ya 40 zilizofanya vizuri kitaifa , miongoni mwa shule tatu ni za mkoa wa Pwani.
Shule hizo na nafasi zilizoshika ni pamoja na Marian Girls (3), Marian Boys (4) na Ahmes(8) ambazo zote zipo wilayani Bagamoyo.
Kwa upande wa watahiniwa waliofanya vizuri zaidi kitaifa na kuwa katika orodha ya kumi bora wanne wanatoka katika shule za Mkoa wa Pwani.
Majina ya watahiniwa hao ambao wote wanatoka shule ya sekondari marian Boys na nafasi walizoshika ni pamoja na Avith G.Kibani(2), Gibson B. Katuma (7), Bryson G Jandwa(8) na Isack Julias(10).
Wanafunzi hao pia wametajwa katika orodha ya watahiniwa wavulana waliofanya vizuri zaidi na kuwa katika kumi bora kitaifa ambapo nafasi zao ni AvithG. Kibani (2), Gibson B. Katuma(3), Bryson G Jandwa (4) na Isack Julias(5).
Kufatia kwa ufaulu huo mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amezipongeza shule hizo kwa kuweza kufanya vizuri na kuingia katika kumi bora.
“Napenda kuzipongeza shule hizi kwa kuweza kufanya vizuri na zimesaidia kuufanya Mkoa wetu wa Pwani kuwa kinara na kushika nafasi ya 7 kwa mwaka huu , ingawa kwa mwaka jana tulikuwa nafasi ya pili kitaifa lakini bado tupo katika kumi bora “ alisema Ndikilo.
Akizungumzia hali ya matokeo katika shule za Serikali Mhandisi Ndiklo alisema kuwa ,nazo zimefanya vizuri katika matokeo hayo kwani hakuna shule hata moja Mkoani Pwani iliyo kwenye orodha ya shule kumi za mwisho, na akasema “shule zetu za Serikali nazo zimesaidia kwa namna moja au nyingine katika kuufanya Mkoa wetu wa Pwani kuingia katika kumi bora , hivyo napenda kuwapongeza walimu wa shule zetu za Serikali pia”.
Aidha Mhandisi Ndikilo amewataka Walimu wa shule za Serikali kujifunza kutoka katika shule za Binafsi zinazofanya vizuri kwenye matokeo ya mtihani katika suala zima la ufundishaji na katoa rai kwa wadau wote wa elimu Mkoani Pwani, kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuzisimamia shule zote za Serikali na kuhakikisha nazo zinafanya vizuri.
Pia amewakumbusha wazazi pamoja na walezi kuwa wanajukumu la kuwalea na kuwasimamia watoto wao ili wapate elimu na kutoliacha jukumu hilo mikononi mwa walimu pekee.
Mkoa wa Pwani umekuwa ukifanya Vizuri katika matokeo ya mitihani mablimbali kwani baadhi ya shule zake na baadhi ya watahiniwa wamekuwa wakipata nafasi za juu katika ufaula na kwa mwaka 2018 ambapo mkoa umeshika nafasi ya 7 kitaifa katika matokeo ya kidato cha nne.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.