• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

Pwani Yazindua Kampeni ya Ugawaji wa Vyandarua Bure Zaidi ya 971,000 kwa Vita Dhidi ya Malaria.

Posted on: July 18th, 2025

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Nsajigwa George, ameongoza uzinduzi wa kampeni ya ugawaji wa vyandarua zaidi ya 971,000 bure kwa kaya 426,637 mkoani Pwani, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutokomeza ugonjwa wa malaria ifikapo mwaka 2030.

Uzinduzi huo umefanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Kibaha, na kuhudhuriwa na wawakilishi kutoka TAMISEMI wakiongozwa na Mratibu wa Malaria Taifa, Stella Kanyange, pamoja na  Peter Gitanya, Afisa Mkuu wa Afya kutoka Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) chini ya Wizara ya Afya. Pia walikuwepo wajumbe wa Kamati ya Usalama, Wakuu wa Sehemu na Vitengo kutoka Sekretarieti ya Mkoa, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Kusirye Ukio, viongozi wa dini na wadau mbalimbali wa afya.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Nsajigwa alieleza kuwa kampeni hiyo itaanza rasmi kutekelezwa kuanzia Agosti 15, 2025, katika kata 108 na vijiji/mitaa 426, ambapo zaidi ya watu 1,633,774 wanatarajiwa kunufaika na vyandarua hivyo vinavyotolewa bure.

Aidha, alibainisha kuwa Mkoa wa Pwani umeendelea kupiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya malaria, ambapo kiwango cha maambukizi kimeteremka kutoka asilimia 15.3 mwaka 2016 hadi asilimia 6.7 mwaka 2022.

“Idadi ya vifo vitokanavyo na malaria imepungua kwa asilimia 27 kutoka vifo 110 hadi 30. Hii ni hatua kubwa ya mafanikio katika mkoa wetu, na ni matokeo ya matumizi sahihi ya vyandarua, unyunyiziaji wa dawa, na usafi wa mazingira,” alisisitiza Nsajigwa.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Dkt. Kusirye Ukio, alisema Mkoa tayari umeanza kampeni ya uhamasishaji kutoka wilaya hadi vijijini ili kuondoa kabisa ugonjwa wa malaria.

Aliongeza kuwa Mkoa umepokea lita 24,000 za dawa maalum kwa ajili ya kuua viluwiluwi vya mbu, ambazo zitatumika kudhibiti mazalia katika maeneo mbalimbali.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Afya – Ofisi ya Rais TAMISEMI, Stella Kanyange alisema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inajivunia mafanikio makubwa ya kupunguza maambukizi ya malaria kutoka wastani wa asilimia 15 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 8.1 mwaka 2022.

“Mapambano dhidi ya malaria yanahitaji ushirikiano wa kila mmoja wetu. Kauli mbiu yetu ni Mimi, Wewe, na Tanzania Bila Malaria ifikapo 2030 – Inawezekana,” alisema Kanyange.

Kampeni hii inaratibiwa kwa pamoja na Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Bohari ya Dawa (MSD), pamoja na Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Magonjwa ya Malaria, Kifua Kikuu na UKIMWI (Global Fund). Lengo kuu ni kuokoa maisha na kujenga jamii yenye afya bora isiyo na malaria.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Madiwani Kibaha na Chalinze Watakiwa Kuimarisha Usimamizi wa Rasilimali za Umma

    January 16, 2026
  • Madiwani wa Kibaha na Chalinze watakiwa Kuwa Mabalozi wa Usimamizi Bora wa Miradi ya Maendeleo

    January 15, 2026
  • Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Afungua mafumzo ya mfumo wa O&D Ulioboreshwa

    January 15, 2026
  • RC Kunenge Atoa Muongozo wa Utekelezaji wa Shughuli za Serikali Mkoani Pwani

    January 09, 2026
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.

  • Situs Toto
  • Situs Slot Gacor
  • AXL777
  • Situs Toto
  • AERO88
  • Situs Slot Gacor
  • DORA77
  • DORA77
  • DORA77
  • Toto Togel
  • Situs Toto
  • AXL777
  • AERO88
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Slot Gacor
  • Situs Toto
  • Toto Slot Gacor
  • Toto Slot
  • Toto Slot
  • KOI200
  • KOI200
  • KOI200
  • Slot Gacor
  • DORA77
  • DORA77
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Toto 4D
  • Toto 4D
  • slot gacor
  • Toto 4D
  • AXL777
  • slot gacor
  • AXL777
  • AXL777
  • AXL777
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • Situs Toto
  • slot gacor
  • toto slot
  • KOI200
  • KOI200
  • KOI200
  • KOI200
  • AXL777
  • AXL777
  • AXL777
  • AXL777
  • Situs Toto
  • slot gacor
  • Toto Slot Gacor
  • AERO88 Slot Gacor
  • Slot Gacor
  • Slot Gacor
  • AERO88
  • Situs Toto
  • situs toto
  • slot gacor
  • situs toto
  • yamitoto
  • kudetabet98
  • kudetabet98
  • yamitoto
  • dora77
  • koi200