Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amepongeza Mkoa wa Pwani kwa kasi kubwa ya maendeleo ya viwanda, akieleza kuwa idadi ya viwanda imeongezeka kutoka 1,387 mwaka 2020 hadi kufikia 1,631 mwaka huu. Hii ni sawa na ongezeko la viwanda 244 ndani ya kipindi cha awamu ya sita ya uongozi.
Mhe. Rais alitoa kauli hiyo leo, Septemba 28, 2025, wakati wa Mkutano wa Kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani.
Amesema kuwa ongezeko hilo la viwanda limechangia kuzalisha ajira 21,149 za moja kwa moja, pamoja na zaidi ya ajira 60,000 zisizo za moja kwa moja.
Aidha, amebainisha kuwa viwanda vidogo vimekuwa na mchango mkubwa katika upatikanaji wa bidhaa zinazotumika ndani ya mkoa.
Aidha, aliongeza kuwa Mkoa wa Pwani kwa sasa una uwezo mkubwa wa kuzalisha bidhaa muhimu za ujenzi zikiwemo saruji, marumaru na mabati ya rangi hatua inayosaidia kujitegemea katika bidhaa za ujenzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.