Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa 2024, Mzava ameeleza, Rais Samia Suluhu Hassan amejipambanua kutoa fedha za kutosha kwenye sekta ya maji ili kusogeza huduma ya maji safi,salama .
Hayo ameyaeleza Leo 30 April wakati akikagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa upanuzi wa maji , ujenzi wa tanki la maji Lita 50,000 kijiji cha Kidomole , Halmashauri ya Bagamoyo Mkoani Pwani mradi ambao utagharimu milioni 176, umefikia asilimia 90 ,utahudumia kaya 700 zenye wakazi 3,660.
Alieleza kwamba , mradi ni mzuri na unaridhisha ila ,kazi zilizobakia zikamilishwe .
"Maji hayana mbadala,kila siku lazima tuguse maji ,kwa umuhimu huo Rais Samia anaendelea kuboresha miundombinu ya maji , kushusha fedha kwenye miradi ya huduma, kujenga miradi ya maji ilihali wananchi wapate huduma na maji safi ,salama yenye uhakika na karibu na mazingira ya wananchi "alisema Mzava.
Vilevile Mzava alisisitiza, watendaji kuendelea kumsaidia mh.Rais katika jitihada zake madhubuti za kuwaletea wananchi Maendeleo na kuinua uchumi.
Nae Mke wa Rais Mstaafu awamu ya nne Salma Kikwete kwa upande wake , alipata fursa ya kumpongeza Rais Samia kwa kazi kubwa anayofanya nchini na kutambulika Duniani kwa weledi wake.
Akipokea Mwenge wa Uhuru katika viwanja vya shule ya Msingi Fukayosi, kata ya Fukayosi, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo kShauri senedautoka Halmashauri ya Chalinze, miradi 15 yenye thamani ya sh.Bilioni 13.7 itatembelewa na kukimbizwa urefu wa km.159.7.
Miradi mingine iliyotembelewa halmashauri ya Bagamoyo, ni sanjali na kukagua mradi wa duka la dawa za jamii hospital ya wilaya na mradi wa barabara , Kitongoji cha Benki ,kata ya Dunda.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.