• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
    • TasksMIS |
    • Events Portal |
Coast Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Pwani

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Mahali tulipo
    • Dira na Dhima
    • Mamlaka
    • Majukumu na Kazi
    • Waliowahi kuwa Mkuu wa Mkoa
    • Waliowahi kuwa Katibu Tawala wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Seksheni
      • Utawala na Raslimali Watu
      • Mipango na Uratibu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Maji
      • Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Manunuzi na Ugavi
      • Ukaguzi wa ndani
      • Uhasibu na Fedha
      • Sheria
  • Wilaya
    • Kibaha
      • Kuhusu kibaha
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Bagamoyo
      • Kuhusu bagamoyo
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mafia
      • Kuhusu Mafia
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kisarawe
      • Kuhusu Kisarawe
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Mkuranga
      • Kuhusu mkuranga
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Rufiji
      • Kuhusu Rufiji
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
    • Kibiti
      • Kuhusu Kibiti
      • Utawala
      • Ulinzi na Usalama
  • Halmashauri
    • H/M Kibaha
    • H/W Kibaha
    • H/W Kisarawe
    • H/W Mafia
    • H/W Mkuranga
    • H/W Rufiji
    • H/W Kibiti
    • H/W Chalinze
    • H/W Bagamoyo
  • Fursa Za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Ardhi
    • Bandari ya Nchi Kavu
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Sera
    • Makala
    • Sheria
    • Hotuba
    • Fomu
    • Mpango Mkakati wa Mkoa
    • Fursa za Uwekezaji
  • Kituo cha Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Maktaba ya Video
    • Nafasi za Kazi

RAS Mchatta Aagiza Miradi ya Maendeleo kukamilika kwa wakati.

Posted on: June 19th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Rashid Mchatta, amezielekeza Halmashauri ya Mji Rufiji na Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti kuhakikisha kuwa miradi ya maendeleo inakamilika kwa wakati na kuleta tija katika kutatua changamoto za wananchi.

Mchatta alitoa maagizo hayo Leo Juni 19 kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, wakati wa vikao vya Baraza la Madiwani vilivyofanyika katika halmashauri hizo kwa ajili ya kupitia na kujadili hoja zilizotolewa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.

Aidha, alizihimiza halmashauri hizo kuimarisha usimamizi wa mapato ya ndani kwa kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha, sambamba na kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo itakayochangia kuongeza mapato na kuimarisha ustawi wa wananchi.

Vilevile, aliagiza kuhakikisha kuwa hoja zote zilizobaki zinafanyiwa kazi na kufungwa ifikapo Septemba, 2025, na kwamba kusiwe na hoja mpya. Alisisitiza umuhimu wa kuwawezesha wakaguzi wa ndani kuzifunga hoja hizo kabla ya kuwasili kwa mkaguzi wa nje.

Katika kuimarisha ukusanyaji wa mapato, Mchatta alielekeza halmashauri zote kutumia mifumo ya kitaifa ya kidijitali kwa asilimia mia moja (100%) ili kuongeza ufanisi na uwazi katika ukusanyaji na matumizi ya fedha.

Akiwa katika Halmashauri ya Mji Rufiji, aliagiza kuwa mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya ndani iendelee kuelekezwa kwenye makundi maalum ili kuwapatia fursa ya ajira na hatimaye kuongeza mapato ya halmashauri.

Pamoja na maagizo hayo, Mchatta alizipongeza halmashauri hizo kwa mafanikio ya ukusanyaji wa mapato na kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo.

Katika hatua nyingine, wenyeviti wa halmashauri hizo walimpongeza Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Pia waliahidi kuhakikisha kuwa hoja zote zilizobaki zitajibiwa kwa wakati.

Naye, Mwakilishi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Mkoa wa Pwani, Pastory Massawe, aliwapongeza madiwani kwa usimamizi mzuri uliowezesha halmashauri kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo. Alisisitiza umuhimu wa kuzuia hoja mpya badala ya kuwa na uwezo tu wa kujibu hoja zilizojitokeza.

Matangazo

  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Baraza la Biashara Mkoa wa Pwani July 04, 2023
  • Uzinduzi wa Program Jumuishi ya Malezi , Makuzi na Maendeleo ya awali ya Mtoto Mkoa wa Pwani October 04, 2023
  • KIKAO CHA BODI YA BARABARA MKOA WA PWANI, OKTOBA 11,2023 October 10, 2023
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAS Mchatta Aagiza Miradi ya Maendeleo kukamilika kwa wakati.

    June 19, 2025
  • Katibu Tawala Pwani Azitaka Halmashauri za Bagamoyo na Chalinze Kudhibiti Matumizi ya Fedha za Umma.

    June 18, 2025
  • Siamini katika kushindwa - RC Kunenge.

    June 17, 2025
  • Kunenge: Pangeni Vipaumbele vyenye tija kwa Jamii.

    June 16, 2025
  • Tazama Zote

Video

Coast Region Investment opportunities
Video Nyingine

Kurasa za Haraka

  • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
  • Hotuba za Mkuu wa Mkoa
  • Mpango Mkakati wa Mkoa
  • Investment Opportunity Profile
  • Taarifa mbalimbali kuhusu Mkoa
  • Maktaba ya Picha
  • Barua pepe za watumishi

Tovuti Zinazoshahabiana

  • OR-TAMISEMI
  • OR - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Wakala ya serikali Mtandao
  • Wizara ya Elimu
  • Baraza la Mitihani la Tanzania

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

Visitors Counter

Location Map

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani

    Sanduku la Posta: 30080 Kibaha

    Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500

    Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500

    Barua pepe: barua@pwani.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.