Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Rashid Mchatta ametoa rai kwa watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo, kufanya kazi kwa uadilifu pamoja na kuzingatia sheria na taratibu za utumishi wa umma ili kuleta tija ndani ya jamii.
Aidha amewasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa ushirikiano na kuacha malumbano maeneo ya kazi.
Rai hiyo ameitoa wakati akifungua kikao cha Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Platinum ,Destiny hall mjini Kibaha.
Mchatta amesema , ili nchi iweze kuwa na maendeleo na kutawaliwa vizuri inapasa watumishi wa umma kufanya kazi kwa uadilifu na weledi ili kuleta maendeleo kwa wananchi .
Katika hatua nyingine, Machatta amempongeza Katibu Tawala Wilaya ya Bagamoyo kwa kuwapeleka watumishi wake mafunzoni na kuwataka Makatibu Tawala wa Wilaya kuiga mfano huo.
Baraza hilo la watumishi lilipitia na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mpango wa bajeti ya mwaka 2022/23 na 2023/24.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.