Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge, ametoa rai kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wao waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2024 wanakwenda shule bila vikwazo.
Aidha amewaasa , viongozi wa Serikali kuanzia ngazi za chini, wahakikishe wanafuatilia wanafunzi hao ,wanaripoti shule kwa wakati.
Akizungumza katika Kikao cha wadau wa elimu mkoa kilicholenga kutangaza matokeo ya Darasa la Saba na kufanya tathimin ya Elimu, kilichofanyika Disemba 28, mwaka 2023, Kunenge amesema suala la elimu katika mkoa ni la kimkakati hivyo jamii, wazazi na viongozi washirikiane kuinua taaluma mashuleni.
Vilevile Kunenge ameeleza, mkoa umejiwekea mkakati, Shule ya Sekondari ya wasichana wenye vipaji ya Bibi Titi Mohammed iliyopo Utete, Rufiji iwe shule inayofanya vizuri katika masomo ya sayansi
Akijinasibu kuhusiana na ufaulu na mafanikio ya sekta ya elimu mkoa ,kwa mwaka 2023, alieleza mkoa huo, umefanya vizuri katika ufaulu wa darasa la 7 kwa asilimia 83.72 ,daraja A ,mkoa ukiwa juu kwa wastani wa kitaifa 3.4.
Pamoja na hilo ,darasa la kwanza na la pili Mkoani humo wamefanya vizuri katika KKK ,kati ya mikoa 26.
Awali ofisa elimu mkoa wa Pwani,Sara Mlaki , alieleza kwa mwaka 2023 wanafunzi wa darasa la saba 41,028 wamefaulu kujiunga na kidato cha kwanza January 2024.
Alieleza, idadi hiyo inajumuisha wanafunzi 189 wenye mahitaji maalum
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.