Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amezihimiza Halmashauri za mkoani humo kutumia sehemu ya mapato yao kuwekeza ili ziweze kujiongezea uwezo wa kuondoa changamoto kwa wananchi.
Akiwa katika baraza Maalum la Madiwani Kibiti na baadae Rufiji yaliyokaa Juni 17, 2022 kwa nyakati tofauti kila moja kwenye eneo lake kupitia na kujadili taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Mwaka 2020/2021, Mkuu huyo wa Mkoa wa Pwani.
“Kazi iliyopo ni kuongeza uwezo wenu, uwezo wa Serikali kupata mapato na kuondoa changamoto za wananchi, tumieni takwimu kuandaa mipango mizuri na Wekeni vipaumbele vyenu sahihi kwani sio kila fedha mnayopata itumike yote.” Alisisitiza RC kunenge.
Akifafanua hali halisi ya uchumi wa Mkoa wa Pwani, Mhe. Kunenge alieleza kuwa takwimu za kiserikali zinaonesha kuwa Mkoa huo unachangia pato la taifa (GDP) kwa asilimia 1.49 na ni wa tatu toka mwisho licha ya kuwa na viwanda vingi.
Pamoja na kuzipongeza halmashauri hizo kwa kupata hati safi, Mhe. Kunenge alisema kuwa utayarishaji mzuri wa mahesabu na kupata hati safi havina mahusiano ya moja kwa moja na uboreshaji na kugusa maisha ya wananchi
kwenye maeneo yao.
Kupata hati safi hakumaanishi kuwa kuna ufanisi ktk kuboresha maisha ya mwananchi na nnafahamu kuwa kuna changamoto ya mapato, mahitaji yanaongezeka, changamoto za wananchi pia zinaongezeka, yanazidi kuwa magumu lakini mkiweka mazingira ya kuibua vyanzo vipya na mikakati mizuri ya ukusanyaji mapato tutafanikiwa.” Aliongeza RC Kunenge.
Kuhusu ukamilishaji miradi inayoendelea kutekelezwa, Mhe. Kunenge alielekeza kila halmashauri kuhakikisha inakamilisha miradi yote na iwe na thamani ya fedha.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.