.Mkuu wa mkoa wa Pwani Mhe Abubakar Kunenge amemuagiza afisa elimu wa Mkoa huo kushirikiana na Wakurugenzi wa halmashauri zote zilizoko katika mkoa huo kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu changamoto zote zinazosababisha kiwango cha ufaulu wa wanafunzi katika mkoa huo kupungua
Rc Kunenge ametoa agizo hilo katika kikao kazi cha tathmini ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2021/22, mkataba wa lishe na uzinduzi wa miongozo hiyo ngazi ya mkoa.
Amesema endapo miongozo hiyo itatekelezwa kwa ufanisi itasaidia , kupunguza changamoto zinazoikabili shule nyingi za misngi na sekondari katika mkoa huo na hivyo kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafuzi.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mkuranga Khadija Nasri ameushauri uongozi wa mkoa kuweka mkakati maalum wa kukabiliana na changamoto zinazoikabili sekta ya elimu ndani ya mkoa huo ikiwemo tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike, utoro na utumikishwaji wa watoto watoto wadogo.
Awali akitoa taarifa juu ya miongozo huo afisa elimu wa mkoa huo Sara Mlaki amesema pamoja na changamoto zinazosababisha wanafunz katika mkoa huo washinddwe kufanya , vizuri katika mitihani yao ya kitaifa , mkoa huo umeanza juhudi mahususi kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa kuratibu kwa mara ya kwanza ufanmywaji wa mitihani ya moko kwa darasa la saba na kidato cha nne ambapo hali ya ufaulu imeonekena kuongezeka kidogo ukilinganisha na mwaka uliopita
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.