Mkuu wa Mkoa wa Pwani ,Mhe .Abubakar Kunenge februari 28,2024 amekutana na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu ,Ummy Nderiananga na kufanya nae mazungumzo yanahusiana na masuala ya mipango na mikakati ya maendeleo mkoani humo.
Kunenge alieleza namna mkoa ulivyojipanga kimkakati hasa katika sekta ya kilimo, uvuvi, ufugaji ,uwekezaji na utatuzi wa migogoro na kero kwa wananchi.
Kuhusu sekta ya kilimo alieleza, mkoa umejikita katika kulima mazao ya biashara na chakula ikiwemo korosho, ufuta, miwa, mihogo, ufuta, pamba na mazao mengine ya biashara.
Nae Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Ummy amempongeza Kunenge kwa mikakati hiyo na kusema kuwa lengo la ziara yake ni kutembelea miradi iliyo chini ya mpango wa AFDP wilayani Bagamoyo.
Akiwa kwenye ziara hiyo alitembelea eneo litakalojengwa chanja la kuanikia dagaa katika soko la samaki la Bagamoyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.