Hayo ameysema wakati Novemba 29,2022 wakiti akitoa akitoa Salaam za Mkoa Wilayani Kisarawe kwenye ziara hiyo amemshukuru Mhe Waziri Mkuu kwa ziara yake ya siku tatu.
"Umetuonesha ni jinsi gani tufanye kazi kama Watumishi wa Umma. Na umetueleza kutambua sisi ni wahudumu wa Wananchi na waratibu wa kutatua Changamoto zao' Kunenge ameeleza Wakati unapita kila sehemu umekuwa ukitoa maelekezo tumeyachukua na tunayafanyia kazi Ameeleza Kunenge.
Ameeleza ataendelea kuhakisha Mkoa unaongeza ukasanyaji wa mapato na kusimamia Matumizi ya mapato yote.
Ameeleza kuwa Mkoa wa Pwani unandaa Mipango ya Bajeti yake kwa Pamoja na Taasisi zote za Serikali ngazi ya Mkoa ili kuwahudumia Wananchi kikamilifu na kutatua kero zao.
Ameeleza atakuwa na Mikataba ya kiutendaji na wakuu bwa Wilaya na Watendaji wengine ndani ya Mkoa kujipima na kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Sita.
Ameeleza kuwa ameelekeza Madiwani wa Mkoa huo wameendelea kwenda mafunzo ya Uchumi na kuongeza Mapato ili wasimamie Halmashauri zao.
Mhe Waziri Mkuu akiwa Wilayan Kisarawe ameetembelea Mradi wa DAWASA, amekagua Ujenzi wa Shule ya Sekondari, Hospital ya Wilaya ya Kisarawe na Jengo la Utwala la Halmshauri ya Kisarawe na Kuongea na Watumishi.
Akizungumza na Watumishi wa Umma Wilayan Kisarawe Mhe Waziri Mkuu, Amewataka Watumishi wote wa Umma kusimamia Miradi inayotekelezwa Mkoa wa Pwani.
Katika Hatua Nyingine amemuondoa Kwenye nafasi ya Ukurugenzi Kaimu Mkurugenzi wa Kisarawe James Chitumbi kwa kushindwa kutekeleza Majukumu ya Ukurugenzi ipasavyo.
Amesisitiza Taarifa za Fedha zimarishwe na kutaka Mapato yote ya Halmshauri yanayokusanywa kupelekwa Benki kabla ya Matumizi..
Amezitaka Halmshauri kusimamia Hojanza CAG zote na kuzjfanyia kazi na Viongozi wa Mkoa Kushughulikia Migogoro ya Wakulima na Wafugaji na kutenga maeneo ya Halmshauri kwa ajili ya Mifugo.
Mhe. Waziri Mkuu akiwa Mkaoni Pwani ameetembelea Wilaya ya Mkuranga, Kibiti na Kisarawe.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.