Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewaelekeza Madiwani wa Halmashauri ya Kisarawe pamoja na watumishi kuhakikisha wanashirikiana katika utekelezaji wa mipango inayowekwa ili kufikisha huduma stahiki kwa wananchi.
Kunenge ameyasema hayo akiwa katika baraza maalumu la Madiwani wa Halmashauri hiyo la kujadili taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG).
Amesema haiwezekani kukawa na ufanisi kama hakutakuwa na ushirikiano kati ya Madiwani na watumishi.
Akiwa katika Halmashauri hiyo Kunenge ametoa maagizo kwa Halmashauri hiyo kuhakikisha wanafunga hoja za ukaguzi.kabla ya June 30.
Mkuu huyo wa Mkoa pia ameagiza madeni yakusanywe ndani ya muda ili kufanya utekelezaji wa mipango iliyolengwa.
Amesisitiza pia utendaji wa haki kwa aliyehusika kuzalisha hoja kuwajibishwa kwa kufuata kanuni na sheria.
Aidha Kunenge ameagiza Halmashauri hiyo kuongeza wigo waukusanyaji wa mapato. “msiangalie vyanzo vya mapato vilivyopo tafuteni vyanzo vingine lakini visiwe vikwazo na kuuwa Uwekazaji.
Katika hatua nyingine kunenge amewataka watendaji kuwekwa kwa mazingira bora ya kukuza wawekezaji.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.