Mkuu wa mkoa wa Pwani mhe. Abubakari Kunenge, ametoa rai kwa kamati ya hamasa na mawasiliano dhidi ya magonjwa ya mlipuko ,wakati inajengewa uwezo katika majukumu yao iweke mpango kazi kushughulikia changamoto kubwa ya ukatili na unyanyasaji ikiwemo kwa wanawake na watoto Mkoani humo.
Akifungua kikao kazi cha kuwajengea uwezo kamati ya hamasa na mawasiliano dhidi ya magonjwa ya mlipuko (RCCE) ,Mkoa na wasilisho la muundo wa kamati hiyo Mkoa na Halmashauri sanjali na majukumu yao, Kunenge alieleza, Mkoa huo bado una shida ya suala la unyanyasaji na udhalilishaji kwa kundi hilo.
Pia, aliipongeza Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na shirika la afya Duniani (WHO) kwa jitihada kubwa wanazozifanya za kukabiliana na magonjwa hayo hatari katika jamii ikiwemo kudhibiti magonjwa ya mlipuko.
Alieleza,baada ya mafunzo hayo kamati hiyo wafuate mfumo wa kutoa ushirikishwaji wa jamii ili kuondoa tatizo la magonjwa ya mlipuko na unyanyasaji na udhalilishaji .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.