Mkuu wa mkoa wa Pwani,Abubakar Kunenge amekagua mahudhurio ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na darasa la kwanza katika baadhi ya shule za sekondari na msingi halmashauri ya Mji Kibaha.
Akiwa shule ya sekondari ya wavulana ya Kibaha, shule ya sekondari Tumbi pamoja na shule ya msingi Amani iliyopo Miembesaba ,Kunenge ametoa maelekezo ya Serikali, kwamba mwanafunzi yeyote asisumbuliwe kuripoti kwasababu ya kukosa vifaa ama sare za shule.
Aidha amewaasa watoto wa kike kusoma kwa bidii na kujiepusha na vishawishi.
Nae Mwalimu mkuu sekondari ya Tumbi, Fidelis Haule alieleza mwamko ni mkubwa, wanafunzi wa kidato cha kwanza wanaotakiwa kuripoti ni 279 ambapo hadi sasa wameripoti 241 .
Akijibu baadhi ya changamoto ikiwemo upungufu wa walimu ,kuongezwa madaraja walimu Ofisa elimu mkoa wa Pwani, Sara Mlaki ameeleza , Serikali inaendelea kushughulikia changamoto mbalimbali ikiwemo kupandisha madaraja walimu .
Mlaki amesema Serikali inatarajia kutangaza ajira kwa watumishi 23,000 nchini ambapo kati ya watumishi hao ni sanjali na walimu .
Mwanafunzi wa shule ya sekondari ya sekondari Kibaha, Moses Damas Canisio amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kujenga mazingira bora ya elimu ,kuongeza madarasa ,kuboresha miundombinu ,kuondoa ada na ujenzi wa mabweni na maabara .
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.