Mkuu wa mkoa Pwani Abubakar Kunenge amewakabidhi Vishkwambi 345 Maofisa Kilimo wa Wilaya za Mkoa huo na kuwataka watumie vifaa kzi hivyo kusidia wakulima uleta tija na kuongeza mnyororo wa thamani.
Zoezi la makabidhiano ya vishikwambii hivyo limefanyika Novemba 23 mjini Kibaha.
Akizungumza mara ya kukabidhi viskwambi hivyo Kunenge amesema kuwa matumizi mengine ni kusajili wakulima ambao bado hawajaingizwa kwenye mfumo na kuboresha taarifa za wale waliosajiliwa ili wahudumiwe kwa idadi na kujua mahitaji yao ya pembejeo.
"Ili kilimo kiwe na tija lazima wataalamu wawe na vifaa vya kisasa na hata iwe rahisi kutoa taarifa juu ya maendeleo ya kilimo au kama kuna changamoto,"amesema Kunenge.
Amesema kuwa kupitia vifaa hivyo wtaweza kutoa taarifa sahihi za pembejeo kwa wakulima kuanzia afya ya udongo, mbegu bora, mabadiliko ya hali ya hewa na matumizi sahihi ya mbolea.
"Tunaipongeza serikali kwa kutoa pikipiki 129, vifaa vya kupimia udongo sita na sasa Vishikwambi hii inaonyesha jitihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan za kutaka kubadili kilimo ili kiwe na tija kwa wakulima na nchi,"amesema Kunenge.
Aidha amesema kuwa mkoa umepata mafanikio makubwa kwa sasa ambapo ubora wa zao la korosho ya daraja la kwanza umeongezeka kutoka asilimia 12 hadi 96.6.
"Zao la ufuta ubora na uzaliahaji umeongezeka na tnaongeza nguvu kwenye mazao yakiwemo katani, mahindi, miwa, mihogo, chikichi, mpunga na mbaazi pamoja na ndizi ambapo tayari kuna wawekezaji wakubwa wameshajitokeza,"amesema Kunenge.
Ameongeza kuwa kikubwa ni maofisa hao kuongeza mnyororo wa thamani kupitia mazao ya kibiashara ambayo yanaongeza pato kwa wakulima.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Shangwe Twamala , amesema wanaishukuru Wizara ya Kilimo kwa kuwapatia vifaa hivyo.
Twamala amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia wakati wa kutoa taarifa mbalimbali kwa Wizara na kutoa elimu kwa wakulima juu ya masuala mbalimbali ya kilimo.
Naye Ofisa Kilimo wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha Joseph Njau amesema kuwa vifaa hivyo vitawawezesha kutekeleza majukumu yao na kuongeza uzalishaji na kuleta tija kwa wakulima kwenye maeneo yao.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.