Mkuu wa Mkoa wa Pwani mhe Abubakar Kunenge leo Agosti 18,2021 amekabidhi Mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Mhe.Amos Makala.
Tukio hilo la Makabidhiano limefanyika katika Viwanja vya Ndege Dar es salaam Terminal I. Awali Mhe. kunenge aliupokea Mwenge huo kutoka kwa Mhe. Mhandisi Martine Ntemo Mkuu wa Wilaya ya
Mafia.
Akitoa salaam fupi wakati wa Makabidhiano hayo Kunenge amesema, Mwenge huo umekimbizwa katika Wilaya zote saba na Kupitia Miradi 87, yenye thamani ya shilingi 57,314,068,446. Ameeleza katika miradi yote iliyopitiwa ni mradi mmoja tu ulikataliwa kutokana na kukosekana kwa nyaraka, ameeleza kuwa wanafanyia kazi Maelekezo yote yaliyotolewa na Mkimbiza mwenge Kitaifa kwenye miradi hiyo.
Kunenge ameeleza pia katika mikesha ya Mwenge watu wengi walijitokeza na hivyo kutekeleza kauli mbiu zingine za kudumu za Mwenge ikiwepo kupambana na maambukizi ya VVU, kutokomeza Malaria, kupambana na Madawa ya kulevya na kupambana na Rushwa.
Kunenge ameeleza kuwa Mkoa wake umetumia mikesha ya Mwenge pia kutoa Elimu na kupima VVU ambapo watu 724 walipimwa na watu 5 tu waligundulika kuwa na maambukizi sawa na asilimia 0.6. Watu 343 walipima malaria, na watu pia walipata fursa ya kuchangia damu kuchangia damu ambapo chupa 35 zilikusanywa.
Ameeleza pia kuwa Elimu juu ya tahadhari ya UVIKO 19 iliotolewa na uhamasishaji wa chanjo ya UVIKO 19 kwa hiari ilifanyika. Ambapo hadi kufikia tarehe 16 Agosti 2021 jumla ya Watu 8328 walichanjwa.
Kunenge amewapongeza wakimbiza Mwenge hao kitaifa kwa uchapakazi wao na ujuzi katika kukagua miradi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.