Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Alhaji Abubakari Kunenge amemuapisha Petro Magoti (Juni 14) kuwa mkuu mpya wa Wilaya ya Kisarawe na kumuagiza kuhakikisha anaweka kipaumbele katika sualazima la ulinzi na usalama katika wilaya hiyo.
Katika halfa hiyo yauapisho imehudhuriwa na viongozi mbali mbali wa serikali viongozi wachama,wakurugenzi,waku wa Wilaya,wakuu wa idara pamoja na wageni wengine .
Mara baada ya kuapishwa,Magoti alitoa shukrani kwa Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwakumuamini na kumchagua katika nafasi hiyo.
Magoti aliahidikushirikiana bega kwa bega na viongozi wa wilaya ya Kisarawe na Mkoa wa Pwanikwa lengo la kuweza kuleta maendeleo kwa wananchi.
“Nashukuru kwa dhati kwaRais kuweza kunichagua katika nafasi hii na mm nitakuwa mstari wa mbele katikakusaidia na viongozi wenzangu katika kuwatumikia wananchi wa Wilaya ya Kisarawe“, alifafanua Magoti.
Vilevile Magoti alieleza,ataonyesha taswira nzuri kwenye uwajibikaji katika uongozi wake na kwambaatayatekeleza yale yote ambayo ameagizwa na Rais kuyatekeleza katika sektambali mbali.
Nchi hii ya Tanzania inawatu wengi sana ambao ni wasomi na wengine wana uwezo mkubwa lakini mheshimiwaRais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeweza kumpendeza na kuamua kunichagua katikanafasi hii na mm namwomba Mungu anijalie niwe mtiifu katika kazi hii,”alielezaMagoti.
Kadhalika Mkuu huyoamemwakikishia Mkuu wa Mkoa wa Pwani kumpa ushirikiano wa kutosha yeye pamojana wasaidizi wake.
Magoti alieleza, katikakutekeleza majukumu yake atahakikisha anafanya kazi kwa weledi kwa kuzingatiamisingi ya kuwa na mshikamano na utiifu.
Mimi nimefanya kaziIkulu na Rais wetu kwa kweli anachapa kazi kweli usiku na mchana maana halalikwa hivyo na sisi viongozi tunapaswa kuiga mfano wake katika kutimiza wajibuwetu,”alieleza Magoti.
Nae Kunenge ametakawakuu wa wilaya kuendelea kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za wananchina kuzitafutia ufumbuzi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.