Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge amepokea mitambo ya kusafisha Maji chumvi (Solar Desalination System) yenye thamani ya Shilingi Milioni 700 zitakazo tumika katika Hospital ya Wilaya ya Mafia na Kibiti.
Akipokea Mitambo hiyo leo Julai Mosi 2022 katika Kituo cha Afya MEDEWEL Kibaha amesema anamshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuweka Mazingira bora ambapo sekta binafsi na wadau mbalimbali wanashirikiana na Serikali katika kutoa huduma kwa Wananchi.
“Kupitia Juhudi hizo leo Mkoa wa Pwani tumepokea mitambo hii ya kusafisha Maji chumvi kutoka kwa wenzetu wa WaterKiosk na Boreal light yenye makazi yake Nchini Ujerumani kwa ufadhili wa benki ya Ujerumani na mitambo hii itatumika katika Hospitali ya Wilaya za Mafia na Kibiti am all mitambo hii itasaidia kusafisha maji chumvi kutoka katika visima vyetu ili kuhakikisha yanakuwa katika hali ya kutumika" alisema RC Kunenge.
Ameeleza kuwa Mitambo iliyokabidhiwa ni mizuri na kwamba ni Teknolojia rahisi inayotumia nguvu ya jua ambayo haina athari katika mazingira na kuwa Mitambo hiyo itahakikisha itaweza kutoa Maji Safi na salama katika bomba na kutumika bila kuweka madawa mengine, pia itasaidia vifaa tiba kudumu kwa muda mrefu kwa kuwa athari za chumvi zitakuwa zimeondolewa.
Akizungumzia upatikanaji maji, RC Kunenge ameeleza kuwa Serikali inafanya Jitihada kubwa kuhakisha maeneo yote yanapata Maji na kwa Mkoa wa Pwani upatikanaji ni wa wastani kwa kiwango cha asilimia 86 na malengo ni kufikia asilimia 95 mijini na asilimia 85 Vijijini ifikapo 2025.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.