Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametaka usimamizi madhubuti wa Mpango Jumuishi wa Wahudumu wa Afya Ngazi ya Jamii ili usaidie kukabili changamoto mbalimbali za kiafya ndani ya jamii.
Kunenge ameyasema hayo leo Mjini Kibaha wakati wa kupitia mpango huo kwa Kamati ya Ulinzi ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, wataalamu wa afya wakiwemo waganga wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri.
Amesema kuwa suala la afya ni muhimu hivyo kuwe na uangalizi na usimamizi madhubuti kwa watoa huduma hao ili uwe na matokeo mazuri ya kukabili na kudhibiti magonjwa kwa wananchi.
"Mpango huu ni mzuri sana na utakuwa na manufaa makubwa kwa jamii lakini kuwe na usimamizi mzuri wa namna mpango huo utakavyotekelezwa ndani ya Mkoa kwani lengo ni kuhakikisha huduma za afya zinawafikiwa wananchi kwa urahisi,"amesema Kunenge
Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Pwani Benedict Ngaiza amesema kuwa kwa sasa Mkoa una wahuduma wa afya ngazi ya jamii 1,025 ambao wako kwenye program za magonjwa mbalimbali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.