Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge ametatua mgogoro wa ardhi baina ya mwekezaji Trans Continental na wananchi wa kata ya Kikongo Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani humo.
Wananchi 214 wa Kata ya Kikongo walilikuta eneo la mwekezaji huyo ambae alikuwa anamiki ene hilo kihalali tangu mwaka 1987 na kuanza kufanya uendelezaji makazi kinyume na sheria.
Kunenge ametoa maamuzi hayo leo Oktoba 30, 2023 kwenye mkutano wa hadhara uliowahusisha Katibu Tawala wa mkoa, wananchi, watalaam wa halmashauri na mkoa.
Amesema hatua hiyo imetokana na jitihada za serikali kutafuta ufumbuzi wa migogoro inayowakabili wananchi.
“Mnatakiwa kufahamu kwamba eneo hili ni mali ya mwekezaji, mmelivamia sasa kwa busara nimemuomba awamegee eneo muanzishe makazi yenu kama kuna mtu hajaridhika anaweza kufuata sheria,” amesema Kunenge.
Mwekezaji wa shamba shamba namba 30/1 Abdrahim Zahran amekubali ombi la Mkuu wa mkoa kutoa eneo kwa ajili ya wananchi waliovamia shamba lake ambapo kila mwananchi atapewa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 500.
Kuhusu eneo kwa ajili ya wananchi hao, amesema watagawa kulingana na vipaumbele vyao kwa sababu wamepanga kufanya uwekezaji wa miradi mingine.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.