Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe. Abubakar Kunenge ,amefanya ziara ya kutembelea Kata ya Kikongo
Halmshauri ya Wilaya ya Kibaha kusikiliza na kutatua kero za Wananchi.
Akitatutua Mgogoro wa Ardhi wa Muda mrefu wa Shamba Na 30/1 na 30/2 Kunenge Ameeleza kuwa Shamba na 30/1 linalomilikiwa na Kamapuni ya Transcontinental halina Mgogoro na Mwekezaji aendelee kuliendeleza na Kwa shamba Na 30/2 ambalo kuna Wananchi ndani amewapa Wataalamu wa Ardhi muda wa mwezi mmoja Kufanya utambuzi wa wote waliomo ndani ya Shamba hilo na kuwasilisha Taarifa.
Kunenge Amesistiza kuwa kila mtu apewe haki yake,"Kama Mwananchi ana haki apewe haki yake kama ni Mwekezaji apewe haki yake" Ameeleza Kunenge.
Kunenge ameeleza ya Kuwa Kuna timu za kushughulikia Migogoro ya Ardhi zilizopo Mkoani hapo ambapo ametaja ni pamoja na Timu kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa inashughulikia Migogoro ya Maeneo ya Jeshi na Wanchi na ipo ndani ya Mkoa huo kwa muda wa siku 52, Timu nyingine na ya Wataalam kutoka Kamishna wa Ardhi inayoshughulikia Migogoro ya Mipaka katika ya Vijiji na Vijijini, Wilaya na Wilaya na Mkoa na Mkoa.
Kunenge amewaeleza Wananchi hao kuwa Migogoro yote itashughulikiwa na kumalizwa ndani ya Mkoa huo na kuwataka wanachi kuzingatia Sheria.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.