Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari kunenge amewataka vijana wa mkoa huo kufanya kazi katika viwanda vilivyopo ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Kunenge ameyasema hayo mwishoni mwa wiki alipotembelea katika eneo ambalo linatarajiwa kuanzishwa kiwanda kipya cha KEDA ceramic katika kijiji cha Msufiji Kata ya Mbezi.
"Serikali haizalishi fedha kutokana na sekta ya Elimu, Barabara wala sekta ya Afya bali ni uwekezaji unaofanyika ambao unaisaidia Serikali kupata mapato pamoja na wananchi kupata fedha na ujuzi," alisema Kunenge.
Awali akiongea na wataalam pamoja na wajumbe wa usalama Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa suala la uwekezaji haliwezi kukwama kwa namna yoyote ile ndani ya mkoa wake kwani haitapendeza kuona Rais Samia Suluhu Hassan akipambana kutafuta wawekezaji alafu tushindwe kuwasimamia ili kufanikisha uwekezaji huo.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ali amewataka viongozi wa kampuni ya KEDA kuishirikisha Halmashauri katika kutekeleza majukumu yao ya kuanzisha kiwanda hicho ili kufanikisha mradi huo ipasavyo.
Kiwanda hicho kinakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 240 hadi kukamilika na kitakuwa cha 3 kwa ukubwa nchini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.