Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewataka Meneja wa Wakala wa Barabara Nchini TANROADS pamoja na Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini TARURA kuwasilishwa maombi yao mapema Ili yaweze kufanyiwa kazi.
Kunenge amesema hayo wakati wa kikao cha Bodi ya barabara kilichofanyika Machi 7 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mjini Kibaha.
Akizungumza katika kikao hicho alisema Taasisi hizo za Serikali zinatakiwa kuainisha na kuwasilisha maombi yao mapema Ili yaweze kufanyiwa kazi kutokana na kuwepo wa miradi mingi inayohitaji fedha.
Awali akiwasilisha taarifa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani Mhandisi Baraka Mwambage aliiwasilisha Makisio ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 sh. 18.9 billion ya matengenezo ya barabara sambamba na sh. 19.4 Bilion fedha za Maendeleo.
Mhandisi Mwambage pia ameeleza kwamba ujenzi wa Barabara ya Tamco Mapinga km 14 unatarajia kuanza hivi karibuni baada ya kupata kibali mwezi Februari mwaka huu.
Ujenzi wa Barabara hiyo utarahisisha usafiri kwa wananchi wanaonda Bagamoyo na Bunju ambao wanalazimika kuzunguka kupitia Mbezi, Tegeta.
Kadhalika amebainisha kuwa usanifu unaendelea kufanywa kupata gharama halisi za ujenzi wa barabara ya Chalinze Utete Km 354.
Amesema katika barabara hiii ujenzi wake utarahisisha kufika mikoa ya Kusini kupitia Chalinze lakini pia kwa wanaoenda bwawa la Mwalimu Nyerere wakitokea Chalinze watapunguza mzunguko sasa.
Hata hivyo vitendo vya baadhi ya wananchi kuendelea kisogea kwenye hifdhi ya barabara na kufanya shughuli zao by vinatajwa kuwa kikwazo kwa Taasisi hiyo.
Naye Meneja wa TARURA mkoa wa Pwani Leopold Runji pia ameaema utekelezaji wa kazi za dharura 2023/2024 mkoa huo imepokea sh.5.8 billion kwa ajili ya kazi mbalimbali za dharura.
Alibainisha baadhi ya kazi za dharura kuwa ni pamoja na kujenga boksi kalavati na kunyanyua tuta barabara ya Rubu-Milona kujenga mawe kuzuia mmomonyoko wa udongo.
Ujenzi wa Barabara km 3 na mitaro kwa ajili ya kuondoa mafuriko mji wa Ikwiriri na kwa Wilaya ya Kisarawe kujenga mitaro na kujaza sehemu ya barabara iliyolika na Mlemba.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.