Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge ,ametoa Rai kwa waandishi wa habari, kutumia kalamu zao kuwaelimisha wananchi mazuri yanayofanywa na Serikali na kutangaza fursa na matarajio makubwa ya mipango ya Serikali.
Aidha amewataka waandishi wa habari kushirikiana na mkoa kutangaza fursa za kiuchumi na uwekezaji zilizopo ili iwe kimbilio la wawekezaji.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Cha Chama Cha waandishi wa habari Mkoani humo, Kunenge alieleza ,endapo wadau ,wangetaka kulipwa gharama ya kazi wanayofanya Basi tusingeweza kurudisha fadhila.
Hata hivyo Alibainisha, mkoa umedhamiria kuufungua Mkoa ,mkoa unakwenda kubadilika katika sekta ya uchumi na uwekezaji.
"Kuna eneo la Kwala ,Tuna kwenda kufungua Mji Kuwa Mji wenye fursa mbalimbali za uwekezaji,Kuna mkakati wa kuboresha Mji huo kwa uwekezaji na kuboresha miundombinu ya maji na umeme hata Bagamoyo tuna kazi kubwa ya kuupanga Mji ,Pia Chalinze, Kibaha, Bagamoyo,Mafia tunakwenda kupima Mji wetu kwa maendeleo ya mkoa"
Alieleza mabadiliko hayo yanatakiwa kutangazwa ,jamii ijue fursa zilizopo hauwezi Kuwa na maendeleo ama mipango yenye fursa zisizojulikana.
Kunenge alifafanua,mipango mingi inajulikana ndani ya jamii kutokana na kushirikiana baina ya Serikali na waandishi wa habari.
"Tunapozungumzia uhuru wa vyombo vya habari,Rais kashaeleza msimamo wa Serikali,Cha kwanza sera,tabia yetu, je tunatenda kulingana na sera na Sheria kanuni na taratibu,! je? tunazitekeleza."
"Muwe sehemu ya kunipatia changamoto, kwakuwa Mimi , napimwa na Rais kutokana na namna ya kusimamia ulinzi na Usalama, kero za wananchi ,,kutatua migogoro mbalimbali, kuisemea Serikali mazuri inayofanya ,"alisema Kunenge.
Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa mkoa alikiahidi chama hicho kukipa kiwanja bure ili kujenga ofisi ya kudumu.
Nae Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Pwani, Ally Hengo alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kupatiwa kiwanja na kusema wanakwenda kuondokana na hali ya kutangatanga.
Alisema, kwa Sasa wamepanga ofisi na kulipa Kodi lakini wakishapata kiwanja hicho na kukijenga itakuwa mkombozi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.