Mkuu wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge amekemea vikali baadhi wafanyabiashara wa Chakula Mkoani humo ,kuacha kugeuza mwezi huu mtukufu wa Ramadhamani ni wa kuvuna Faida kwa kuongeza Bei ya vyakula kiholela.
Hayo ameyasema wakati akizindua msikiti wa Masjid E Mariya na kugawa Futari kwa Ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhani vilivyotolewa na Taasisi ya kiislam ya Miraaj Tanzania April 20 2022 huko Visiga Kwa Kipofu,Kibaha.
RC Kunenge aliwataka wafanya Biashara hao kuacha kuongeza Bei za vyakula ukizingatia Ni mwezi wa Toba Jambo ambalo sio jema na linasababisha manung'uniko ndani ya jamii.
Aidha, Mhe. Kunenge aliiasa, jamii kuzingatia elimu ya dini kwani ndio urithi kwa watoto wetu kwa maisha yao baadae.
Kunenge amemshukuru aliyetoa eneo la msikiti Allah atamlipa kulingana na alichokitoa kwa Ajili nyumba ya Ibada, alihimiza amani kuhakikisha amani inapatikana kuanzia ngazi ya chini kuanzia Mm kusaidia ujenzi wa msikiti.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani
Sanduku la Posta: 30080 Kibaha
Simu ya Mezani: 023 2402287/2402500
Simu ya Mkononi: 023 2402287/2402500
Barua pepe: barua@pwani.go.tz
Hakimiliki ©2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani. Haki zote zimehifadhiwa.